Posts

Tambua faida ya matumizi ya Choya (rosela) kiafya

Image
Rosela ni ni maua yanayo julikana kabisa  pia  huoeshwa au kupandwa mazingira ya kawaida haswa nyumbani, maua haya yanapatikana kirahisi katika nyumba za ndugu, jamaa na marafiki na sehemu zinginezo japo kuwa baadhi ya watu huyaita maua damu. Zifuatazo ni faida za kutumia rozela. Maua ya rosella utengenezwa juisi inayo ongeza damu mwilini kwa haraka Hutumiwa kama mboga na mbegu zake hutoa mafuta yanayo tumika kama dawa ya vidonda. Dawa ya magonjwa mbalimbali kama kushusha presha, sukari, uric acid mwilini, inatibu kikohozi na mafua, ina punguza mwili pia hutengeneza ngozi na kuifanya iwe laini. Maua ya rosela hutumika kutengenezea juisi , chai ,jam, pia hutumiwa kama rangi ya chakula. Faida zinginezo; Maua ya rosella yana vitamin C,A,D B1,B2,calcium,magnesium,iron, nk Muhimu. Kulingana na matumizi na faida za maua ya rosella ni vyema kupanda kwa wingi maua haya katika mazingira ya nyumbani kama ya navyo pandwa maua mengine ili iwe rahisi kuyapata pindi yanap

BREAKING NEWS: Rais Magufuli amteua Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

Image
 Rais John Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) kuchukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Valentino Mlowola ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Mabasi Mawili ya Wanafunzi Yagongana, Dereva Afariki

Image
Muonekano wa basi la shule ya Kivulini baada ya ajali. Basi la shule ya Nyamunge likionekana baada ya ajali. Mabasi mawili ya wanafunzi ya Shule za Kivulini na  Nyamunge yamengana uso kwa uso katika Barabara ya Mwanza–Simiyu katika eneo la Nane Nane mkoani Mwanza na kusababisha kifo cha dereva na wanafunzi wanane wa shule hizo kujeruhiwa.

Wakili wa kesi ya Mbowe na wenzake ajitoa

Image
WAKILI Jeremiah Mtobesya aliyekuwa akiwawakilisha Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na viongozi wenzake nane wa chama hicho, amejitoa kwenye kesi hiyo leo Agosti 23 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri. Mtobesya amejitoa katika kesi hiyo baada ya Mahakama ya Hakimu Kisutu kutupilia mbali maombi yao ya kutaka kesi hiyo ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 iahirishwe katika Mahakama ya Kisutu ili kusubiri  maombi yao na rufaa yaliyowasilishwa kwenye Mahakama ya Rufani yasikilizwe kwanza na kutolewa maamuzi. Kwa upande wake, hakimu Mashauri alitupilia mbali maombi hayo kwa maelezo kwamba, kifungu cha sheria walichotumia cha 225 (1) (2) cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 hakiipi mamlaka hayo. Ikumbukwe kwamba, Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwamo  kuhamasisha maandamano Februari 16 mwaka huu siku moja ya uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni yaliyosababisha

NAFASI ZA KAZI 45 HOSPITALI YA BUGANDO

Image
OFISI ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetangaza nafasi 45 za kazi Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza za Medical Attendant daraja la II, mwisho wa kutuma maombi ni 2018-08-29 MEDICAL ATTENDANT II.. – 45 POST Employer: Bugando Medical Centre Date Published: 2018-08-15 Application Deadline: FASI DUTIES AND RESPONSIBILITIES: i. Providing basic health education to in patients and relative ii. Ensuring that all utensils are clean. iii. Inspecting the Institute clinical areas. iv. Advising matron on all matters relating to cleaning duties. QUALIFICATION AND EXPERIENCE: Holder of an Ordinary Secondary School Certificate. Must have a Pre-Nursing Certificate OR Certificate in Community Health from recognized institution REMUNERATION: Salary Scale PMOSS.2.1. Login to Apply

Irene Uwoya ampa za uso shabiki Instagram

Image
 Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na akanti nyingi ‘fake’ za Instagram ambazo zinatumia majina ya mastaa na viongozi wa serikali na usipokuwa makini unaweza kugombana na kila mtu mtandaoni. Kwani akaunti hizo zimekuwa zikitumiwa na watu hao kwaajili ya kuwachonganisha mastaa kwa mastaa ili wapate followers. Hayo yamemkuta malkia wa filamu, Irene Uwoya baada ya kuingia kwenye majibizano na akaunti ‘fake’ ambayo inatumia jina la Jokatemwegeelo akidhani anabishana na Mhe DC Jokate, ambae kupitia mtandao huo anatumia jana Jokate Mwegelo. Kaunti hiyo ‘fake’ ilionekana ikidai muigizaji huyo wa filamu amekuwa akitumia muda mwingi kwenye kujiremba na sio kufanya kazi.

RC Mongella ashiriki mazishi ya Bibi yake Paul Makonda

Image
Na James Timber, Mwanza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella leo Agosti 23, ameungana na waombolezaji mbalimbali kushiriki mazishi ya Bi. Anna Makwega Manasse (81) ambaye ni Bibi wa Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda. Mazishi ya Bi. Manasse ambaye alifariki dunia juzi Agosti 21, Mwaka huu akiwa katika hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu, yamefanyika katika makaburi ya nyumbani yaliyopo Kahangala wilayani Magu. Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa serikali mkoani Mwanza, Mkuu wa Mkoa Mongella amewaombea kuwa na uvumilivu kwa  ndugu, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo na kuwahimiza kumuombea kwa Mola ili apumzike kwa Amani.

Haji Manara Awapa Makavu Mashabiki wa Simba

Image
Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara. Msemaji wa klabu ya Simba mwenye mbwembwe nyingi miongoni mwa klabu za soka nchini, Haji Manara, ameibuka kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuwapa makavu mashabiki wa Simba wanaoponda ushindi wao bao 1-0 dhidi ya Prisons walioupata jana uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo uliofungua pazia la Ligi Kuu mwaka huu. Alichokisema:- Wakati mwingine najiuliza nn wanadaamu wanataka?hasa washabiki wa Mpira!! Nimetalii kdogo kwenye magroup machache ya Wanasimba kwenye WhatsApp nimeshangaa baadhi yetu kutokuridhika na ushindi wa leo wa goli moja dhidi ya Prisons Wengine kwenye Instagram wanafika mbali zaidi eti mfumo wa kocha haufai!! Guys mpira ni sayansi kubwa kuliko kwenda mwezini au daktari kumfanyia upasuaji wa kichwa mtu,ukubwa wa Sayansi hii ni kwamba hujui mpinzani wako kajipangaje..hujui kama siku hyo wachezaji wako watacheza kwa kiwango gani lakini kubwa Sayansi hii haina jawabu la moja kwa moja kam

Diamond uso kwa uso na Rich Mavoko

Image
Msanii wa muziki wa kizazi kipya na C.E.O wa lebo ya WCB Wasafi Diamond Platinumz leo amekutana uso kwa uso na aliyekuwa msanii wake Rich Mavoko katika ofisi za baraza la sanaa Tanzania Basata. Diamond wamekutana na Mavoko katika ofisi hizo kwa lengo la kuongelea tofauti zao ambazo zimejitokeza kwa kile kinachodaiwa kuwa Rich Mavoko amejitoa katika lebo hiyo. Mavoko alijiunga na WCB mwaka 2016 akisaini chini ya lebo hiyo na kuanza kufanya kazi akiwa chini ya lebo hiyo ambayo boss wake ni Diamond Platinumz. Baada ya kujiunga na lebo hiyo Mavoko alianza malalamiko mapema mwaka huu kuwa anataka kujitoa katika lebo hiyo ya WCB wasafi kwa madai kwamba ananyonywa kimaslahi. Mbali na kunyonywa kimaslahi lakini pia ilidaiwa kuwa kuna vitu ndani ya makataba huo msanii huyo hakutimiziwa na boss wake kama mkataba ulikuwa unaelekeza. Malalamiko ya Mavoko yalionekana kuwagusa wengi na ikachangia Mavoko kukaa kimya kwa muda ingawa siku za hivi karibuni aliachia ngama yake

Uwoya awawashia moto wanaomsakama kuhusu Dogo Janja

Image
Mwanamama wa tasnia ya filamu za Kibongo, Irene Uwoya amejikuta akiwaka baada ya kuhojiwa sababu za kutomposti mumewe, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa zamani. Akizungumza na Risasi Jumamosi, Uwoya ambaye inadaiwa kuwa hayuko sawa na mumewe huyo alidai kuwa siyo lazima kila mara atamposti kwani ana mambo mengi ya kuandika na atafanya hivyo endapo tu imebidi. “Siyo kila mara nitakuwa natumia kurasa zangu kumposti Dogo, nina mambo mengine ya kufanya pia, itakapobidi kufanya hivyo nitafanya,” alisema Uwoya akionekana kuna jambo haliko sawa.  Uwoya alihojiwa hayo baada ya kila mara kuonekana akiposti picha za kuwa ndani ya ndege ambapo wapo waliosema kuwa kwa sasa amekuwa akisafiri na kumuacha mumewe huyo peke yake. “Siyo kweli, mimi sisafiri mara kwa mara, zile ni picha tu nimewahi kusafiri mara moja nilipokua nikienda Mwanza kwenye Miss Lake Zone,” alisema Uwoya

Uwoya awawashia moto wanaomsakama kuhusu Dogo Janja

Image
Mwanamama wa tasnia ya filamu za Kibongo, Irene Uwoya amejikuta akiwaka baada ya kuhojiwa sababu za kutomposti mumewe, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa zamani. Akizungumza na Risasi Jumamosi, Uwoya ambaye inadaiwa kuwa hayuko sawa na mumewe huyo alidai kuwa siyo lazima kila mara atamposti kwani ana mambo mengi ya kuandika na atafanya hivyo endapo tu imebidi. “Siyo kila mara nitakuwa natumia kurasa zangu kumposti Dogo, nina mambo mengine ya kufanya pia, itakapobidi kufanya hivyo nitafanya,” alisema Uwoya akionekana kuna jambo haliko sawa.  Uwoya alihojiwa hayo baada ya kila mara kuonekana akiposti picha za kuwa ndani ya ndege ambapo wapo waliosema kuwa kwa sasa amekuwa akisafiri na kumuacha mumewe huyo peke yake. “Siyo kweli, mimi sisafiri mara kwa mara, zile ni picha tu nimewahi kusafiri mara moja nilipokua nikienda Mwanza kwenye Miss Lake Zone,” alisema Uwoya

JPM Apiga Marufuku Wamachinga Kunyanga’nya Bidhaa

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Njia panda ya Bugando mjini Mwanza wakati akiwa njiani kuelekea Chato mkoani Geita. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Sengerema mkoani Mwanza kuelekea Chato mkoani Geita. Rais Dkt. John Magufuli amewapiga marufuku viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kuwanyang’anya bidhaa wafanyabiashara wadogo na badala yake amewaagiza viongozi wote nchini kujielekeza katika kutatua kero zinazowakabili wananchi. Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo Agosti 18, 2018 alipokuwa anasalimiana na wananchi waliokusanyika mjini Sengerema akiwa njiani kuelekea Chato Mkoani Geita kwa mapumziko, ambapo wananchi hao walidai halmashauri ya Wilaya hiyo imekuwa ikiwanyang’anya matunda aina ya nanasi wakulima na wafanyabiashara wanaouza matunda yao mjini hapo. “Nilishasema viongozi wote niliowateua mimi msishereheke

KIFO CHA MAJUTO… KILICHOMTOA FAHAMU TAUSI CHA JULIKANA

Image
S IRI ya muigizaji Tausi Mdegela, kuangua kilio kupita kiasi kwenye msiba wa nguli wa vichekesho Bongo, Amri Athuman ‘King Majuto’ wiki iliyopita imebainika kuwa msanii huyo alikuwa ni baba yake wa hiari aliyemfundisha sanaa ambayo sasa inamweka mjini. Akizungumza na Ijumaa wa Wikienda, Tausi alisema kuwa, Majuto alikuwa baba yake aliyemlea katika maadili mema na aliyetamani sana kumuona anafika mbali kisanaa kwani ndio aliyemfundisha na alikaa naye nyumbani kwake Tanga kwa muda mrefu kama mwanaye wa kumzaa. “Mimi hapa nalia kwa uchungu mkubwa naumia mno kumpoteza baba yangu aliyenilea katika kazi kwa sababu ni mtu ambaye alikuwa anataka kujua hali yangu kila mara na alipenda mno kuona maendeleo yangu kila siku kama mwanaye,” alisema Tausi. Akiendelea kuzungumza na gazeti hili kwa uchungu, Tausi alisema kuwa Mzee Majuto hata wakati anakaribia kufariki yeye alikuwa ametoka nje kidogo ya Jiji la Dar lakini alipigiwa simu na dairekta Leah Mwendamseke ‘Lamata’ na ku

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO YA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Agosti, 2018 amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya 1, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 41, na amewahamisha vituo vya kazi Mkuu wa Wilaya 1 na Wakurugenzi wa Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 19. Taarifa iliyotolewa leo tarehe 13 Agosti, 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe. Dkt. Magufuli amemteua Bi. Senyi Simon Ngaga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mkoa wa Mwanza. Bi. Senyi Simon Ngaga amechukua nafasi ya Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato Mkoani Geita, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Chato aliyeteuliwa hivi karibuni Kanali Patrick Norbert Songea kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi nje ya nchi. Uteuzi wa Bi. Senyi Simon Ngaga unaanza leo tarehe 13 Agosti, 2018 na Wakuu wa Wilaya wote wawili wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao

RAIS MAGUFULI APONGEZA JIMBO LA MBULU KUPATA ASKOFU MPYA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria profesa Palamagamba Kabudi na Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti na viongozi mbalimbali wakifuatilia misa Takatifu ya kumweka wakfu Askofu wa Jimbo la Mbulu Anthony Lagwen. Askofu wa Jimbo la Mbulu Anthony Lagwen akiwekwa wakfu kuwa askofu wa Jimbo hilo mjini Mbulu Mkoani Manyara jana. Askofu wa Jimbo la Mbulu Anthony Lagwen akiwa kwenye kiti chake baada ya kusimikwa kushika nafasi hiyo mjini Mbulu Mkoani Manyara jana, kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Dar es salaam mhadhama Polycap Kardinali Pengo na Askofu mwandamizi Yuda Thadeus Ruwaichi. Waziri wa Katiba na Sheria profesa Palamagamba Kabudi akimkabidhi Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu Anthony Lagwen, zawadi iliyotolewa na Rais John Pombe Joseph Magufuli baada ya Askofu huyo kusimikwa jana mjini Mbulu Mkoani Manyara. RAIS John Magufuli amewapongeza wananchi wa wilaya za Mbulu, Babati na Hanang’ mkoani Manyara na Karatu mkoani Arusha zin

WASANII WAJITOKEZA KUMUAGA MZEE MAJUTO

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz (mwenye kanzu nyeupe) akibeba jeneza la mwili wa aliyekuwa nguli wa filamu za uchekeshaji nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’ baada ya kumalizika kwa shughuli ya kuuaga mwili wake iliyofanyika leo tarehe 9 Agosti, 2018 kwenye viwanja vya Karim Jee vilivyoko jijini Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz akibeba jeneza la mwili wa aliyekuwa nguli wa filamu za uchekeshaji nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’. Msanii wa Bongo Movie, Jacob Steven ‘JB’ akizungumza na wanahabari wakati wa shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Mzee Majuto.  Msanii wa Bongo Movie, Single Mtambalike (wa kulia) akizungumza na msanii mwenzake, Mzee Hashim Kambi (wa kushoto).

Rich Mavoko Ashinda Kesi Dhidi ya WCB

Image
EXCLUSIVE: Msanii Rich Mavoko ameshinda kesi ya kujiengua katika Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB). Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa katika Ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania ( Basata). Takribani miezi miwili iliyopita taarifa zilianza kusambaa kuwa Mavoko ametimuliwa WCB huku nyingine zikieleza kuwa amejiengua mwenyewe. Aidha, viongozi wa lebo hiyo hawajataka kuweka bayana kinachoendelea dhidi ya Mavoko ambapo hivi karibuni, Mmoja wa viongozi hao, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ hivi karibuni alikaririwa akisema wakati wa kuzungumzia jambo hilo haujawadia.

Spika Wa Bunge Apokea Barua Ya Kujiuzulu Kwa Mbunge Wa Monduli

Image
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amepokea barua ya kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiuzulu Ubunge wa Jimbo la Monduli kutoka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Julius Kalanga.

Shamsa: Akinipenda Chidi Inatosha!

Image
Shamsa Ford STAA mwenye mvuto Bongo Muvi, Shamsa Ford amesema kuwa hata kama leo watu watamchukia kwa jinsi alivyo au kwa kuzungumza ukweli hawezi kuumia hata siku moja kwa sababu anaamini aliyempenda kwa dhati ambaye ni mumewe Chidi Mapenzi yupo, inatosha. Staa huyo alizungumza na gazeti hili la Amani baada ya watu wengi kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kutokelezea na nguo fupi kwenye 40 ya mtoto wa Zamaradi, na kusema kuwa ni ngumu kumridhisha kila mtu kwenye maamuzi yako. “Mimi Mungu kanijalia maneno sijali kabisa na isitoshe Chidi akinipenda na akakubaliana na maamuzi yangu kwangu inatosha kabisa siwezi kumridhisha kila mtu,” alisema Shamsa.

MKUU WA WILAYA YA ARUMERU, JERRY MURO AFANYA ZIARA ARUSHA

Image
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Jerry Muro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Meru na Arusha.  MKUU wa Wilaya ya Arumeru, Mheshimiwa Jerry Muro jana tarehe 01 Agosti, 2018 alifanya ziara ya kikazi pamoja utambulisho kwa watumishi wa Halmashauri Mbili za Meru yenye kata 26 na Arusha  yenye kata 27 zilizo katika Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha. Akiwa katika halmashauri hizo, Mhe. Muro aliwataka watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia mahitaji ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo ndio anasimamia Utekelezaji wake katika halmashauri zote mbili zenye kata 53.  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Jerry Muro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Meru na Arusha.  Katika Ziara Hiyo, Mhe Muro aliambatana na Mkuu wa wilaya ya Monduli, Mhe Iddi Hassan Kimanta aliyekuwa akikaimu Wilaya ya Arumeru, pamoja na Katibu Tawala, Bwana Timotheo Mzava pamoja na baadhi ya viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya