Posts

Showing posts from May 3, 2017

SPIKA JOB NDUGAI ATOA MAANA YA "FALA"BUNGENI

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai jana ameonyesha aliumizwa na kitendo cha Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya CHADEMA Mh. Halima Mdee kumwambia 'fala' bungeni na kusema hata kama mtu humpendi lakini si vyema kumtusi matusi. Job Ndugai alisema hayo alipokuwa akitoa maana ya neno fala bungeni ambapo ilibidi arejee maana hiyo kwa kusoma kupitia kamusi ya Kiswahili ambayo ilitoa maana kuwa fala ni mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri. "Kwa neno ambalo alilisema Halima Mdee humu ndani, kamati imeenda kwenye tafsiri ikachukua Kamusi kwa neno lile alilosema ambalo maana yake kwa yule unayemwambia 'Fala' ni mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri, ni mtu mpumbavu, ni mtu bwege, ni mtu mjinga, ni mtu bozi, ni gulagula. Ndiyo maana nikasema sisi Waafrika hata kama humpendi namna gani mwenzako huwezi kumfanyia hivyo"  alisisitiza Job Ndugai

Dk Mwakyembe: Televisheni, Redio kusoma vichwa vya habari tu kwenye magazeti kuanzia kesho

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe   Mwanza.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amezitaka Televisheni na Redio kuanzia kesho kusoma vichwa vya habari vya magazeti tu ili kuwavutia wasomaji kununua magazeti kwa habari kamili. Dk Mwakyembe amesema hayo leo jijini Mwanza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini ambapo pia amesema ataendelea kutetea na kulinda haki za waandishi wa habari huku akiwahakikishia ulinzi waandishi wa habari za uchunguzi. Pamoja na mambo mengine Dk Mwakyembe amehakikisha kuwepo kwa ushirikiano wa kutosha kwa wamiliki wa vyombo vya habari  na kwamba ameagiza idara ya mawasiliano kutengeneza mawasiliano ya kudumu na wawe wanakutana angalau mara moja kwa mwezi kujadili udhaifu unaoweza kujitokeza na kuchukua hatua lengo ni kuwekana  sawa.

SAMATTA AMEANZA KUIKAMATA KRC GENK, SHABIKI AINGIA NA BANGO AKIOMBA JEZI

Image
Ukisema mambo yanaanza kunyooka, baada ya mashabiki wengi wa KRC Genk kuonyesha imani kubwa kwa mshambulizi, Mbwana Samatta.Samatta anaonekana kuwa bora zaidi kutokana na kuwa tegemeo katika kikosi cha Genk cha Ubelgiji.Imeonekana mmoja wa shabiki akiwa na bango uwanjani, akiomba jezi ya Samatta.Imekuwa kawaida kwa mashabiki wa Ulaya kuomba jezi kwa wachezaji wanaowapenda wakitumia mabango kama shabiki huyo wa Genk. Samatta amekuwa akifunga mfululizo na wakati mwingine kushindwa kufanya hivyo kwa kipindi fulani lakini imani kwa benchi la ufundi na mashabiki inaonekana kupanda kwa kiwango cha juu kabisa.

CHADEMA wateua majina mapya ya Wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki

Image
Chadema wafanya uteuzi wa wagombea Ubunge EALA.   Tazama majina yao: 

Faida za Mchaichai kiafya

Image
Faida za mchachai zipo nyingi sana wengi wetu hudhani mchaichai ni kuongo cha kuweka kwenye chai pekee, au ni dawa kwa ajili ya kuua mbu pekee, ila mchaichai huwa na faida lukuki zaidi ya hizo tu. Naomba uweze kusoma makala haya ili uone faida nyinginezo za mchaichai. Zifuatazo ni faida za kutumia mchaichai kiafya. 1. Mchaichai ni kinga dhidi ya saratani. Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani. Mwaka 2006, timu ya watafiti kutoka Chuo kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai un uwezo wa kuua seli zinaweza kusababisha saratani. 2. Hutibu magonjwa ya kuhara. Husaidia umeng’enyaji wa chakula Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo kujaa gesi. Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini Katika matibabu, unatibu magonjwa mengi ikiwemo kushusha joto, hasa

BAJETI YA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO YAPITISHWA

Image
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati), akimsikiliza Katibu Mkuu (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Kulia), mara baada ya kumaliza kuwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2017/2018. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipongezana na Watendaji wa Wizara hiyo mara baada ya kumaliza kuwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2017/2018. Watendaji wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakipongezana mara baada ya Bunge la Bajeti kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2017/2018. Mtendaji Mkuu Wa Shirika la Reli Nchini (TRL), akizungumza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju mara baada ya Bunge la Bajeti kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2017/2018. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilia

KAULI YA EMMANUEL MBASHA BAADA YA FLORA KUOLEWA TENA

Image
Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Emmanuel Mbasha, ambaye alikuwa mume wa Flora ameweka wazi kuwa hana shida na Mume mpya wa madam Flora Daudi Kusekwa.  Kupitia eNewz ya EATV, Emmanuel Mbasha amesema kuwa hana shida na mume mpya wa Flora kwani yeye hamfahamu na kama akikutana naye hawezi kumfanya lolote maana huyo mtu hakuwahi kumuingilia katika ndoa yake, ila Mbasha akasema mtu ambaye yeye anamchukia ni yule aliyeingilia ndoa yake ambaye Watanzania wanamjua. "Sijaona kama nimepungukiwa, jamaa ambaye amemuoa Flora sina shida naye, anaweza kuwa mtu ambaye ananihofia kuwa nikikutana naye naweza kumdunda. Ila huyo jamaa mimi simchukii na wala simjui.Hajawahi kuniingilia kwenye issue yangu yoyote ya mapenzi ila mimi namchukia jamaa ambaye aliniingilia kwenye ndoa yangu ndiye mbaya wangu, na Watanzania wote wanamjua." Alisema Emmanuel Mbasha.  Mbali na hilo Emmanuel Mbasha alisema kuwa Flora amemkimbia kutokana na maisha aliyoyachagua lakini si

Spika aziweka rehani ajira watumishi Bunge

Image
SPIKA WA BUNGE, JOB NDUGAI. SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, ametishia kuwafukuza kazi watumishi wanne wa Bunge wanaofanya kazi kwenye ofisi za Kambi Rasmi ya Upinzani ikiwa wataendelea kuandika hotuba alizoziita zenye maneno machafu dhidi ya uongozi wa Bunge. Aliyasema hayo bungeni jana wabunge walipoazimia kuwasamehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (Chadema) waliokutwa na hatia ya kukidharau chombo hicho cha kutunga sheria. Ndugai mbali na kuipongeza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kazi nzuri ya kuwahoji viongozi hao waliolalakiwa, alisema amebaini kuna ‘mchezo mchafu’ dhidi ya uongozi wa Bunge unaofanywa na wanaoandika hotuba za upinzani. Alisema hotuba kadhaa za upinzani zimekuwa na maneno yanayoashiria kudharau Bunge, hasa Kiti cha Spika. “Nimefanya utafiti wangu. Kw