Posts

Showing posts from April 10, 2017

Mbunge Hussein Bashe atumiwa ujumbe wa Vitisho, Usome hapa...

Image
Mbunge wa Nzega Vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hussein Mohamed Bashe amesema kuwa ametumiwa ujumbe wa vitisho na watu wasiojulikana wakisema kuwa watamfanyika kitu kibaya popote pale alipo. Bashe ambaye yupo kwenye vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma ameandika leo asubuhi kupitia akaunti yake ya Tiwtter kuwa, ametumiwa ujumbe huo uliosomeka, “Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale tulipo.” Kufuatia vitisho hivyo, Mbunge Hussein Bashe amelitaka Bunge na Serikali kutofumbia macho vitendo hivi vya wananchi kutekwa na watu wasiojulikana. Vitisho hivi kwa mbunge huyo vimekuja ikiwa ni siku chache tu tangu mwanamuziki Roma Mkatoliki na wenzake watatu walipotekwa na watu wasiofahamika wakiwa katika studio za Tongwe Records jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS MH. MAMA SAMIA SULUHU HASSAN APOKEA KIFIMBO CHA MALKIA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kifimbo cha Malkia kutoka kwa bondia Haji Matumla, Ikulu jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kupokea kifimbo cha Malkia kuashiria uzinduzi wa michezo ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika Australia Aprili 2018, jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kupokea kifimbo cha Malkia kuashiria uzinduzi wa michezo ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika Australia Aprili 2018, jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Haya ndio Majibu ya Halima Mdee kwa Gwajima

Image
Mbunge wa Kawe Halima Mdee amejibu kile alichotuhumiwa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Askafu  Josephat Gwajima kuwa anamuheshimu sana  mchungaji huyo. Mdee ameelza kwenye akaunti yake ya Twitwer kuwa hakumtukana Spika wa bunge na wala hatarajii kumtukana @halimamdee Namuheshimu sana Mch.Gwajima,sitajibizana nae kwenye mitandao. Niweke rekodi sawa sijamtukana na wala sitarajii kumkosea heshima Spika.  https:// twitter.com/mitandaonblog/ status/851079630094299136  … 7:13 PM - 9 Apr 2017  ·  Dodoma, Tanzania     37 37 Retweets     204 204 likes  Follow Halima James Mdee   @halimamdee Hayo ya J2 namwachia yeye! Yangu na yaliyojiri Bungeni.. Najua jinsi ya kuyahandle. Yawezekana yalishamalizwa kabla ya Ibada yake LEO.  https:// twitter.com/mitandaonblog/ status/851079630094299136  … 7:17 PM - 9 Apr 2017   ·   Dodoma, Tanzania ...

7 wasimamishwa kazi kwa ubadhirifu wa mil 900/-

Image
Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Hussein Ruhava HALMASHAURI ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imewasimamisha kazi watendaji waandamizi na wakuu wa idara saba wa manispaa hiyo kwa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha ya halamshauri hiyo ya Sh milioni 900. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Hussein Ruhava alisema kuwa maamuzi hayo yamefanyika kupitia kikao cha fedha na uongozi cha halmashauri hiyo kilichofanyika mjini Kigoma. Meya Ruhava alisema kuwa maamuzi hayo ya kamati ya fedha na uongozi yametokana na taarifa ya mkaguzi wa ndani inayoonesha kuwepo kwa matumizi yanayotia shaka ya kiasi cha zaidi ya Sh milioni 900 ambazo maelezo yake na vielelezo vilivyopo vinatia shaka. Pamoja na hilo ametoa agizo kukamatwa na kuhojiwa kwa baadhi ya watalaamu kwa madai ya kughushi nyaraka na kujipatia fedha isivyo halali. Aliwataja waliosimamishwa kuwa ni pamoja na mhandisi wa ujenzi Boniface William, mhandisi msaidizi wa uj...