Posts

Showing posts from August 7, 2017

Rais Kagame Amjibu Rais Magufuli Twitter

Image
Rais wa Rwanda amejibu tweet ya dr John Pombe Magufuli , aliyomwandikia kwa ajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa tena kwa awamu nyingine kuwa rais wa Rwanda. ANGALIZO; Inaonekana hawa viongozi wawili wametokea sana kuelewana mpaka kufikia hatua Paul Kagame kumwita rais Magufuli ndugu yangu, hongera sana Rwanda na Tanzania kwa mshikamano huu. Replying to @MagufuliJP Nakuahidi kuuendeleza Undugu na ushirikiano wetu katika nyanja zote kwa ajili ya maendeleo ya nchi zetu. Replying to @MagufuliJP Kwa niaba ya Wananchi wa Rwanda na kwa niaba yangu binafsi, nakushukuru sana Ndugu yangu Mheshimiwa Rais

RAIS DKT. MAGUFULI AREJEA JIJINI DAR ES SALAAM NA KUHUTUBIA WANANCHI WA BUNJU B

Image
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Bunju wakati akirejea jioni ya leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano katika mkoa wa  Tanga.   Baadhi ya wananchi wa eneo la Bunju wakimsikiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza aliposimama eneo hilo kwa ajili ya kuwasalimia  wakati akirejea jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano katika mkoani    Tanga. PICHA NA IKULU

Rais Magufuli Agoma Kukaa Madarakani Miaka 20

Image
Rais John Magufuli akiwahutubia  wananchi. amesema hawezi kukaa madarakani kwa miaka 20 kwa kuwa anaheshimu Katiba na kwamba kazi ya urais ni ngumu. Magufuli amesema hayo leo Jumatatu, Agosti 7 katika Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga alipozungumza na wananchi na kuzindua stendi ya kisasa ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya siku tano mkoani humo. Kauli hiyo ya Rais imekuja baada ya Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani ‘Prof. Maji Marefu’ (CCM) kusema kwa kuwa Magufuli anafanya kazi nzuri na ingekuwa vizuri akiongezewa hata miaka 20. “Nadhani Profesa Maji Marefu unataka niishi miaka 20 zaidi na siyo kuwa rais kwa miaka 20, sitafanya hivyo kwa kuwa naheshimu Katiba,” alisema Magufuli.

Aveva, Kaburu hali tete

Image
Kesi inayowakabili Rais wa Simba Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange 'Kaburu' imehairishwa hadi Agosti 16 mwaka huu kutokana na kuwa upelelezi hujakamilika dhidi yao. Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Victoria Nongwa ambapo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ambayo mawili kati ya hayo ni ya utakatishaji fedha. Viongozi hao walikamatwa na TAKUKURU miezi miwili iliyopita kutoka sasa wakikabiliwa na mashitaka ya kutakatisha fedha mpaka kupelekea kunyimwa dhamana.

Waziri Mwijage Afunguka Baada JPM Kutoridhishwa na Utendaji Wake

Image
Waziri Mwijage (kulia) akiwa kwenye kipindi cha Clouds 360 kufafanua yaliyosemwa na rais Magufuli jana. Jana (August 6, 2017) Rais Magufuli  alitoa kauli ya kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji dhidi ya watu waliouziwa viwanda na kuvitelekeza ambapo alimtaka Waziri Mwijage kuwanyang’anya na kuwapatia wawekezaji watao viendeleza. Leo August 7, 2017 Waziri wa Viwanda Charles Mwijage amehojiwa kwenye Clouds 360 Clouds TV na kuelezea kuhusu hiyo kauli ya rais na kutoa hizi kauli. ”Kujenga viwanda sio mchezo, yapo maelekezo ya Rais viwanda vilivyo binafsishwa na havitumiki virudishwe, Rais alichokitegemea kwangu sio kile anachokiona sababu viwanda haviendi kwa kasi anayoiona na hii kuna sababu kadhaa.   “Hii sekta ya viwanda ni multi-sector maana kuna viwanda vipo chini ya Wizara ya Mifugo, vingine maliasili…. kuna viwanda vimechukuliwa lakini havipo kwenye orodha ya viwanda vilivyobinafsishwa, nahitaji Wak...

RAIS DKT. MAGUFILI AZINDUA STENDI MPYA NA YA KISASA YA MABASI MJINI KOROGWE LEO

Image
 Taswira za Stendi mpya na ya kisasa ya mabasi mjini Korogowe mkoani Tanga ambayo imezinduliwa asubuhi hii na Rais Dkt. John Pombe Magufuli

PENZI LA GWAJIMA, FLORA JIPU PWAA!

Image
Askofu Gwajima. TAKRIBAN miaka miwili iliyopita kuliibuka sarakasi ya aina yake  katika ndoa ya waimba Injili wawili Bongo, Emmanuel Mbasha na Flora Mbasha ambazo zilisababisha mastaa hao kutalikiana mahakamani. Katika sakata hilo, Mbasha alishusha tuhuma nzito zisizobebeka kwamba Flora alikuwa na uhusiano wa kimapenzi (penzi la Gwajima Flora) na baba mchungaji wao ambaye ni Askofu wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church almaarufu Ufufuo na Uzima, Dk Josephat Gwajima. KIMYA KIREFU Baada ya tuhuma hizo palipita kimya kirefu bila ufafanuzi toshelezi wa skendo hiyo ‘hevi’ lakini kwa mara ya kwanza, Flora amepasua jipu pwaa juu ya ni nini kilichotokea. Kupitia kitabu chake ambacho Ijumaa Wikienda lina nakala yake kilichoingia sokoni wiki iliyopita, pamoja na mambo mengine yasiyoandikika gazetini, Flora alimtuhumu Mbasha kwa mambo mazito ikiwemo hilo la kumpa penzi Askofu Gwajima. TUJIUNGE NA FLORA “Wakati tatizo lile linatokea tulikuwa tunasali kw...

Mzee wa Upako kumbadili dini Q-Chief?

Image
Msanii wa muziki wa bongo fleva Q Chief ambaye hivi karibuni ameachia ngoma yake mpya ya 'Naogopa', amezungumzia suala la kubadili dini na kuingia kwenye dini nyingine, baada ya kuwa karibu na mchungaji Anthony Lusekelo. Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Q Chief amezungumzia suala hilo na kusema huwa familia yake upande wa mama ni Wakristo na ana amini katika Mungu, lakini sio rahisi kwake kubadilisha imani yake. "Familia yangu upande wa mama wengi ni wakristo, lakini wamegawanyika kutoka kwenye uislam kwenda ukristo, baba yangu ni muislam, babu yangu ana msikiti kwa hiyo sio jambo jepesi kutoka kwenye dini yangu imani yangu kwenda kwenye imani nyingine, naamini Mungu ndiye jibu sahihi, lakini huwa nachukua ushauri wa viongozi wa dini tofauti tofauti", alisema Q Chief Q Chief aliendelea kwa kuzungumzia kitendo chake cha kuwa karibu na Mchungaji Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako', na kusema Mchungaji huyo ni sawa na ka...