FAHAMU HUU UMUHIMU WA MASSAGE KWA MWILI WAKO
Je, kuna siku umewahi kuamka asubuhi na kujikuta ukiwa mchovu sana kupita kiasi? hivi ulihisi nini baada ya kuamka hivyo? Je, ulihisi una kahoma kidogo? au uliwaza huenda ni uchovu wa kazi za jana yake? naamini kuna mengi ulijiuliza na huenda hukupata jibu la uhakika. Kwa kawaida huwa kuna sababu nyingi za mtu kuamka akiwa mchovu wa mwili, miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na uchovu wa kazi, michezo n.k. Lakini unaweza kuepukana na hili suala la kuamka na uchovu endapo tu utajenga utaratibu wa kupata huduma ya kukandwa ( massage ) mwili kila baada ya muda fulani. Huduma hii ni vyema ukafanyiwa na mwezi (mke au mume) wako nyumbani ikiwa unahitaji kufanya kwa lengo la kuweka mwili wako sawa sawa tu. Mtaalam wa masuala ya 'massage' kutoka Mandai Herbalist Clinic Mathayo Masinema Bahebe anasema kuwa massage husaidia kupunguza na kuondoa maumivu yote ya mwili pamoja na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini na kuweka sawa sehemu zote za maungio ya mifupa ...