NASSARI: Maisha Yangu Yapo Kwenye Bonde la Uvuli wa Mauti
Nassari na Lema. MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki (CHADEMA) Joshua Nassari amefunguka na kusema maisha yake yapo hatarini na kudai kuwa watu ambao amewaanika kwenye sakata la ununuzi wa madiwani wanamtafuta. Nassari amesema hayo ikiwa imepita siku moja toka alipokwenda kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupeleka ushahidi wake juu ya madiwani wa CHADEMA waliohama chama kwa kuhongwa rushwa na wateule wa Rais John Pombe Magufuli. “Maisha yangu yapo kwenye bonde la uvuli wa mauti, Maisha yangu yapo hatarini kwani Watesi wetu wananitafuta” aliandika Nassari kupitia ukurasa wake wa Facebook. Mbali na hilo wachangiaji mbalimbali kwenye ukurasa wa Mbunge huyo walimtaka azidi kumuomba Mungu huku wakimshauri kuongeza ulinzi zaidi katika maisha yake ya kila siku kutokana na jambo ambalo ameliibua na kumtaka aendelee kupambana, baadhi ya wachangiaji wengine wamedai kuwa anachofanya ni njia ya kujitafutia umaarufu kisiasa. Juzi M...