Posts

Showing posts from May 18, 2018

DONGOBESH FC YAICHAPA STAND FC YA HAYDOM GOLI 1-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KURUGENZI CUP 2018

Image
 Mchezaji wa timu ya Dongobesh FC Antipas Vicent akiwa amebebwa juu juu na mchezaji mwenzake mara baada ya kumalizika kwa mchezo katika yake na timu ya Stand FC ya Mjini Haydom ambapo mchezaji huyo ndiye aliyeifungia timu yake goli 1-0 na timu ya Dongobeshi kufanikiwa kuingia nusu fainali katika michuano ya Kurugenzi Cup 2018 linaloandaliwa na Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom.ikidhaminiwa na Kiwanda cha maziwa cha ASAS cha Iringa, na benki za NMB na CRDB.  Wachezaji wa timu ya Dongobash FC wakisikiliza maelezo ya Mmoja wa Waratibu wa michuano hiyo Bw. Phars Nyanda wakati akiwapa utaratibu mara baada ya mchezo huo kumalizika.  Benchi la Ufundi la Timu ya Dongobesh FC likinyanyuka juu na kushangilia mara baada ya kuifunga timu ya Stand FC ya mjini Haydom katika mchezo uliofanyika leo jioni kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom.  Golikipa wa timu ya Stand...

Ukiwa na sifa hizi, kila mwanaume atatamani kukuoa!

Image
KUOLEWA ni heshima kwa mwanamke. Heshima hiyo inaenda mbali zaidi hadi kuwagusa wazazi wa binti ambaye ataolewa. Wazazi wanatembea kifua mbele pindi binti yao anapoolewa, tena wanafurahia zaidi binti huyo anapoolewa akiwa angali bado hajazaa. Wanamshukuru Mungu kwa binti yao kujitunza. Wanamshukuru binti kwa kuwapa heshima katika familia yao na ndiyo maana siku ya sherehe ya kuagwa (send off) wazazi wanafurahi sana kuagana na binti yao kwa heshima. Hali hiyo huwa inaleta shauku kubwa kwa warembo wengi kutamani kuingia kwenye ndoa. Wengi wanaguswa na rekodi za wanawake wenzao ambao wamejitunza na hatimaye kuwaletea heshima wazazi wao. Kinyume chake, wengi wamejikuta wakijilaumu kwa kushindwa kuleta heshima katika familia zao. Binti umri unaenda, anatamani kuingia kwenye ndoa lakini hapati wa kumuoa. Au mwingine inatokea, anatamani kuolewa lakini anaishia kupigwa mimba na kuachwa. Badala ya kuleta heshima, analeta aibu katika familia yake kutokana na mila na destu...

VIDEO QUEEN MBARONI KWA WIZI

Image
M UUZA sura kwenye video za Kibongo ‘Video Queen’ aliyejipatia umaarufu kwa kutupia picha za utupu mitandaoni, Agness Mmasi, yamemkuta mazito, baada ya kuswekwa rumande kwa tuhuma za utapeli Ijumaa linakumegea ishu kamili. Akipiga stori na Ijumaa, chanzo wa kuaminika kilieleza kwamba muuza sura huyo, mpaka juzi (Jumatano), alikuwa bado akisota rumande katika Kituo cha Polisi Mabatini Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa takribani siku nne. “Mnahabari kamba Agness amedakwa kisa kutapeli nguo maeneo ya Kijitonyama? Kama hamjazidaka ni kamba alichukua kwa mkopo, baadaye akawa anamzungusha mwenye mzigo, mara amtukane hapo ndipo alipodakwa na mpaka sasa anasota nyuma ya nondo,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta anayedaiwa kuwa ndiye mwenye mzigo huo wa nguo ambazo Agness alichikichia nazo, aliyefahamika kwa jina moja la Nyange na alipopatikana alikiri kutapeliwa na mwanadada huyo. “Ni kweli alichukua mzigo wa ngu...