Gwajima ataka Bunge lisimame kuombeleza vifo vya wanafunzi 32
Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephath Gwajima amemtaka Spika wa Bunge kuahirisha kikao cha Bunge siku ya kuaga miili ya watoto waliofariki kwa ajali ya jana. Amesema kama Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliamuru viongozi kusimama kwa kuwakumbuka watoto hao itakuwa ajabu kwa bunge kuendelea na vikao vya Bunge Amesema Spika akiahirisha Bunge kwa siku moja itatoa nafasi kwa wabunge hao kwenda Arusha ili kuomboleza pamoja.