Posts

Showing posts from May 10, 2016

Yatazame hapa: Majina ya kashfa ya kuficha fedha ughaibuni (Panama Papers) yawekwa wazi.

Image
Kashfa ya kuficha fedha ughaibuni (offshore) maarufu kama Panama Papers imechukua muelekeo mpya baada ya shirika la uandishi wa kiuchunguzi duniani (ICIJ) hii leo kuweka wazi majina na nchi za vigogo wanaohusika na kashfa hii. Kufahamu kuhusu wahusika Tanzania na nchi nyingine bonyeza hapa . Facebook Comments

DKT KIKWETE ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE KIGAMBONI

Image
Mweneyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipewa maelezo ya awali na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alipowasili kukagua daraja lla Nyerere, leo Mei 10, 2016. Kulia ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka. Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Joseph Nyamhanga, akimpokea Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipowasili kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na viongozi mbalimbali waliompokea, kabla ya kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama barabara zinazopishana ya chini na ya juu mwanzoni mwa daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo, leo Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama barabara zinazopishana ya chini na ya juu mw...

WAZIRI MKUU: SERIKALI ITAAGIZA TANI 70,000 ZA SUKARI

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Waandishi wa Habari kwenye makazi yake jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaagiza kutoka nje ya nchi tani 70,000 za sukari ambapo kati ya hizo, tani 11,957 zimeshawasili nchini na zitaanza kusambazwa kesho (Jumatano). Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Mei 10, 2016) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam. Akitoa ufafanuzi wa sukari ambayo imekwishawasili nchini, Waziri Mkuu alisema tani 2,000 zitapelekwa mikoa ya Kaskazini, tani 3,000 (mikoa ya Kanda ya Ziwa), tani 2,000 (mikoa ya Kusini), tani 2,000 (Nyanda za Juu Kusini) na tani 2,000 (mikoa ya Kanda ya Kati). “Tani nyingine 24,000 za sukari zitawasili Ijumaa hii na hadi zitoke bandarini itakuwa kama Jumapili kwa hiyo zinaweza kusambazwa kuanzia Jumatatu. Tani nyingine 20,000 zitawasili baadaye, ama mwishoni mwa mwezi...