Mpango wa kumtimua Zitto Kabwe ndani ya CHADEMA wafichuka....
Habari yako Mpekuzi. Kuna mpango wa kumung'oa Zitto kwenye nafasi yake ya naibu katibu mkuu- CHADEMA ambao ulisukwa kiufundi sana ndani ya kikao kilichoitishwa na Mbowe... Nimekuwa nikihangaika sana kuufichua ukweli bila mafanikio.Jana niliiweka habari hii JF lakini waliitoa kwa maslahi yao binafsi....Naomba ujumbe huu uwafikie wanachama wote wenye mapenzi ya dhati na Chama chetu. Kikao hicho kilifanyika nyumbani kwa Mbowe katikati ya mwezi octoba mwaka huu na kilihudhuriwa na LEMA, MNYIKA, SUGU, WENJE, MSIGWA na BAUNSA mmoja aitwaye SWAI, Katika kikao kile Mbowe aliwadhihaki wabunge wake aliokuwa nao kikaoni kwa kusema wanamuogopa zitto na kwamba amewakalia kichwani...