RAIS MSTAAFU, MHE. DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA WANAFUNZI NA WANACHAMA WA CCM WAISHIO JIJINI BEIJING - CHINA.
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akijiandaa kuzungumza na Wanafunzi na wanachama wa CCM waishio Mji wa Beijing nchini China. Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, akizungumza na wanafunzi na Wanachama wa CCM, waishio nchini China, wakati alipokutana nao akiwa katika ziara yake nchini humo. ************************************** Na Mwandishi Wetu, Beijing China Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe 20th April 2016 amekutana na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Tawi la Beijing ambao ni Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, katika Ukumbi wa Grand uliopo katika Makazi ya Viongozi ya Diaoyutai State Guesthouse jijini Beijin, nchini China. Wakisoma risala yao, Wanafunzi hao kutoka vyuo mbalimbali vilivyopo Beijin na miji ya karibu kama vile Tianjin walimuhakikishia Mheshimiwa Dkt. Kikwete kuwa wao ni waaminifu na w...