HAFLA FUPI YA KUWAAPISHA MAWAZIRI WAPYA IKULU DAR LEO
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal wakiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri Mbalimbali wapya mara baada ya kuwaapisha kwenye viwanja vya ikulu leo ambapo viongozi mbalimbali wa serikali na waalikwa wamehudhuria na kushuhudia Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akiwa na mkewe aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Faraja Kotta na familia yake, baada ya kuapishwa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kulia kwa Makamu ni Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba. Picha na OMR Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Adam Malima, kuwa Naibu Waziri wa Fedha, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri Mbalimbali wapya na wanaohamia katika wizara nyingine mara baada ya kuwaapisha kwenye viwanja ...