KIVUKO CHA MV DAR ES SALAAM KUANZA KAZI HIVI KARIBUNI
Rais Dk. John Pombe Magufuli akikagua kivuko cha MV Dar es salaam. Na Raymond Mushumbusi MAELEZO Kivuko cha Mv Dar es Salaam maarufu kama kivuko cha Rais Magufuli kipo katika matengenezo ya kawaida na kinatarajiwa kuanza kutoa huduma kama kawaida siku za hivi karibuni. Akitoa ufafanuzi juu ya madai ya kutelekezwa kwa kivuko cha Mv Dar es Salaam katika maegesho yaliyopo kigamboni Jijini Dar es Salaam ,Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Manase Le-Kujan amesema sio kweli kwamba kivuko hicho cha Mv Dar es Salaam kimetelekezwa bali kimepumzishwa kutokana na matengenezo yaliyohitajika kufanywa katika kivuko hicho ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wasafiri. “Sio kweli kwamba Kivuko cha Mv Dar es Salaam kimetelekezwa katika maegesho ya Kigamboni bali kimepumzishwa kwa muda kwa ajili ya matengenezo yake ya kawaida, hii ikiwa ni juhud i ya kukiwezesha Kivuko hiki kuwa katika ubora unaotakiwa katika kutoa huduma...