TAMKO LA RAIS MAGUFULI KUFUTA SAFARI ZA NJE,VIKWAZO VITANO VYA TAJWA
Agizo la Rais John Magufuli la kusitisha safari za nje linakabiliwa na ugumu katika utekelezaji wake kutokana na nchi kuwa na balozi 36 tu ambazo zitatakiwa kufanya kazi maeneo mbalimbali duniani. Muda mfupi baada ya kuapishwa na kuanza utekelezaji wa majukumu yake ya mkuu wa nchi, Rais alifuta safari zote za nje kwa watumishi wa Serikali na viongozi ili kuokoa fedha zinazotumika kwa ajili hiyo na kuagiza shughuli hizo zifanywe na mabalozi. Rais alisema safari hizo zitadhibitiwa na Ikulu ambayo itatoa kibali kwa safari maalumu, ikiwa ni pamoja na kuweka masharti ambayo mtumishi anayetakiwa kusafiri atatakiwa kuyatimiza kabla ya kupewa kibali. Lakini utekelezaji wa agizo hilo unakabiliwa na vikwazo vingi, hasa vikubwa vitano ambavyo ni uchache wa balozi za Tanzania nje ya nchi, ukomo wa madaraka ya mabalozi, wigo wa ufahamu wa mambo ya kitaalamu na ukosekana kwa mazungumzo endelevu iwapo suala moja litawakilishwa na watu wawili tofauti kwenye mikutano miwili tofauti. Takwimu za Umo...