Posts

Showing posts from February 1, 2018

Figa Ya Sasha Yazua Utata

Image
Sasha Kassim. KALIO la muuza nyago wa video mbalimbali za wanamuziki Bongo, Sasha Kassim limezua utata kwa kudaiwa kuwa si halisi. Chanzo kimepenyeza ubuyu kuwa, Sasha amekuwa ‘akijiedit’ kupitia simu yake hivyo watu kumuona ana kalio kubwa tofauti na uhalisia. Sasha akionyesha figa yake bomba. “Wewe kutana naye hivi laivu halafu utaniambia,” alisema mtoa ubuyu. Alipoulizwa Sasha kuhusiana na hilo alisema; “Siwezi kuwazuia watu kuongea sifoji kitu mimi, siri kubwa ya shepu yangu ni mapozi kwenye picha na aina ya mavazi ninayovaa.”

RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Omar Makungu, , Naibu spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mhe George Mkuchika katika picha ya pamoja na viongozi wa dini na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuhutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya w...

Msigwa afunguka haya Bungeni

Image
Kamatakamata ya viongozi wa vyama vya siasa, wakiwemo wabunge leo Februari1, 2018 imemuibua bungeni Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kusema vitendo hivyo ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Msigwa ameibua hoja hiyo katika kipindi cha maswali na majibu, baada ya kuulizwa swali la nyongeza akihoji sababu za wanaokamatwa kushikiliwa kwa muda mrefu katika vituo vya polisi. “Mimi ni mhanga wa jambo hili napenda kujua msingi wake ni nini, lini mambo haya yatakoma,” amesema. Mbunge huyo amehoji lini taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu ambayo ilieleza kuhusu kamatakamata itawasilishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa. Akijibu suala hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde amesema “..,  naomba wananchi wawe watulivu na kujiepusha kufanya mambo yasiyofaa.” Amesema kwa mujibu wa Katiba, tume hiyo inapaswa kuwasilisha taarifa zake kwa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya haki za binadamu. ...

Ridhiwani atoa agizo afisa mtendaji kuondolewa mara moja

Image
Chalinze.  Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete ametaka kuondolewa mara moja kwa ofisa mtendaji wa kata ya Vigwaza, Elizabeth Msenga kwa maelezo kuwa ameshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Ridhiwani ametoa kauli hiyo leo Februari1, 2018 katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini humo, kutaka mtendaji huyo kupangiwa eneo jingine la kazi. Amesema haiwezekani wananchi wanapata matatizo na kukosa mtu wa kuwasikiliza na kuwasilisha kero zao sehemu husika. “Yaani akija mbunge ndio wananchi wanalalamika jukwaani. Uzembe huu unasababisha wananchi kuwa na hasira na kukichukia CCM wakidhani hakiwasilizi na hakiwajali kumbe ni uzembe wa mtu mmoja tu,” amesema na kuongeza, "Nimezunguka vijiji zaidi ya vinne kero zinazopewa ni nyingi lakini utatuzi wake upo chini ya Serikali ya kata. Nashangaa hata ofisa mtendaji hayupo katika ziara na si mara ya kwanza, hakuna taarifa ya Serikali iliyoandaliwa.” Wakati ombi lake la kutaka ofisa huyo kuondolewa l...

TLS wammwagia sifa Rais Magufuli

Image
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Godwin Ngwilimi amepongeza Rais  John Magufuli kwa kutekeleza matarajio ya watanzania.  Ngwilimi ametoa kauli hiyo leo Februari mosi jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria na uzinduzi wa mwaka mpya wa kimahakama. Pia, ameomba uwezeshaji wa rasilimali fedha katika muhimili wa mahakama ili kushughulikia changamoto zinazoikabili. "Kama chama cha mawakili, tunakuunga mkono na tunaahidi kutoa ushirikiano kwa mahakama pale inapostahili." Ametoa wito akisema, watumishi wa mahakama, majaji, wasajili, watendaji , makarani  na watumishi wengine, mawakili, wanasheria popote walipo wanatakiwa  kutambua mwelekeo wa nchi unabadilika kwa kasi, matarajio ya wananchi , kuondokana na utamaduni wa kuendelea kufanya kazi kimazoea, kutumia fursa zilizopo ikiwamo Tehama ili kuboresha huduma kwa wananchi. Pia  kuendelea kusimamia maadili ya kitaaluma na uadilifu , hat...

Lulu Diva arudisha mahari

Image
MWANAMUZIKI wa kike anayekuja kwa kasi Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amerejesha kwa mikono yake mwenyewe mahari aliyokuwa ametolewa na mchumba wake aliyedumu naye kwa takriban miaka mitatu. Chanzo chetu makini kilisema kuwa, mwanamuziki huyo alikuwa afunge ndoa mwishoni mwa mwaka jana lakini kutokana na kuvuja kwa habari kuwa anatoka na mwanamuziki mwenziye wa Bongo Fleva, mwanaume huyo akadai mahari yake. “Kama kuolewa basi Lulu angeolewa mwaka jana mwishoni lakini mchumba huyo alibaini anatoka kimapenzi na mwanamuziki mwenzake akaomba mahari yake irudishwe,” kilisema chanzo. Gazeti hili lilipompigia simu Lulu na kumuuliza madai hayo alisema, ni kweli alirudisha mahari lakini si kwamba mwanaume huyo alijua anatoka na mwanaume mwingine bali alipata shinikizo kutoka kwa ndugu zake. “Aliposhinikizwa sana nikaona isiwe tabu nikamrudishia mahari yake kwa maana alikuwa akiwasikiliza sana ndugu zake ambao walikuwa hawataki anioe,” alisema Lulu. Na Imelda Mtema

BREAKING NEWS: KAMPUNI YA TTCL “YAFUTWA”

Image
Kampuni ya Mawasiliano Tanzania ya (TTCL), sasa haipo tena, imebadilishwa na kuwa Shirika la (TTCL Corporation). Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa, amesema kuwa anamshukuru sana Rais Magufuli kwa kuona umuhimu wa kuona wa kuwa na shirika la mawasiliano madhubuti kwa ajili ya kuleta maslahi mapana ya nchi, huku akitoa shukrani pia kwa Wabunge wote kwa kukubali kupitisha muswada huo. Aidha Prof Mbarawa, amesema uwepo wa sheria ya shirika la mawasiliano unatoa fursa ya kuboresha sekta kwa kuweka mazingira mazuri ya usimamizi wa miundombinu ya mikakati chini ya shirika hilo. Profesa Mbarawa pia amewajulisha Watanzania wote kuwa mabadiliko ya kuhama kutoka kampuni kuwa shirika la mawasiliano hayatawaathiri kwa namna ya utoaji wa huduma mbalimbali ambazo zilikuwa zinatolewa na kampuni ya simu ya (TTCL) huku akielezwa kuwa wanaodaiwa na iliyokuwa kampuni hiyo watatakiwa kulia madeni yao kama mikataba yao ina...

RAIS WA UGANDA AGUSWA NA KIFO CHA MSANII RADIO

Image
Kufuatia kifo cha msanii wa muziki Radio aliyefariki alfajiri ya leo nchini humo, Rais wa Uganda Yoweri Museven ameonyesha hisia zake kwa kuguswa na kifo cha msanii huyo. Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Museven ameandika “Have been told about the untimely death of musician Moses Ssekibogo aka Mowzey Radio. I had only recently made a financial contribution towards his treatment and hoped he would get better. He was a talented young person with a great future ahead of him. May he rest in peace.” Taarifa za kifo cha msanii huyo zinakuja baada ya siku chache zilizopita Rais Museven kutoa kiasi cha Milioni 30 kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo. Vile vile wasanii mbalimbali kama Navio, Diamond, Eddy Kenzo, Professa Jay na wengineo wametumia kurasa zao za mitandao yao ya kijamii kama Instagram na Twitter kutoa pole kwa familia yake. Baada ya kutangazwa taarifa za kifo mashabiki wa msanii huyo na wa Goodkife walifika hospitali hapo kushuhudia kinachoendele...