Posts

Showing posts from September 8, 2017

Je unajua vyoo vya kukaa vina madhara kiafya kwa watumiaji

Image
Nyumba haiwezi kuwa kamili bila kuwa na huduma hiyo ya choo, Hata hivyo, pamoja na umuhimu wa choo, lakini si kila nyumba iliyo na choo au hata zile ambazo zina huduma hiyo, basi vyoo ni vibovu, havina hadhi. Zipo aina mbalimbali za vyoo kwa matumizi ya binadamu katika maisha yake ya kawaida. Vyoo vina matumizi mengi ingawa  bado  watu wengi  hasa katika nchi maskini na zinazoendelea ikiwamo Afrika wanatumia choo cha kuchuchumaa wakati wa kujisaidia, lakini mijini na katika nchi zilizoendelea, wao hutumia vyoo vya kukaa. Nyumba nyingi mijini na ofisi mbalimbali zinazojengwa hivi sasa, huwekewa vyoo vya kukaa. Hata zile za zamani zinakarabatiwa na kubadilishwa kwa kuwekewa hivi ambavyo vinaonekana vya ‘kisasa’. Mgunduzi wa vyoo vya aina hii, Thomas Crapper anasema kwa mtazamo wake aliona kukaa wakati wa kujisaidia ni utambulisho wa ustaarabu na maendeleo. Hata hivyo, madaktari wanapingana naye wakisema kujisaidia katika vyoo vya kukaa kuna madhara kiafya kwa k

ANGALIA PICHA YA KWANZA MADAKTARI WALIOKOA MAISHA YA TUNDU LISSU

Image
                       Timu ya Madaktari waliookoa uhai wa Mh Lissu kwa huduma ya dharula Mjini Dodoma wakiwa chini ya Dr. Mpoki(Katibu Mkuu W/Afya), Dr. Mponda (Orthopaedic), Dr. Samwel (Orthopaedic),na Dr. frank.Mh Lissu tayari ameondoka katika ardhi ya Tanzania na kwenda Nairobi Kenya kwa matibabu zaidi akiambatana na mkewe kipenzi wakili msomi Alicia Lissu sambamba na Mwenyekiti wa Chadema Mh. Freeman Mbowe, na Mh. Peter Misigwa.