Posts

Showing posts from May 29, 2014

HIZI NDIO PICHA NA LIST YA WASANII WA BONGO MOVIE WALIOFARIKI WAKIWA BADO NA UMRI MDOGO SANA!!

Image
RECHO: Hapa ndipo atakapo anza siku yake ya kwanza leo kwenye makazi yake mapya mbinguni. Shimo dogo ni kaburi ya mtoto wake aliyefariki muda mfupi baada ya kumzaa! RECHO: KUZALIWA 1988  KUFARIKI: 2014. UMRI: 26YRS KUAMBIANA: Hapa ndipo yalipo makazi ya milele ya Adam Kuambiana aliyefariki wiki iliyopita, leo akitimiza siku ya 13 kwenye makazi yake mapya  KUAMBIANA: KUZALIWA:  1976 - KUFARIKI: 2014  UMRI: 38Yrs JOHN MAGANGA: Haya ni makazi ya John Maganga akiwa leo naye anatimiza mwaka mmoja na miezi 6 JOHN: KUZALIWA: 1988 KUFARIKI: 2012 UMRI: 24Yrs MALISA: Haya ni makazi ya milele ya msanii mwingine Malisa ambaye ameshatimiza mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu atutoke ZUHURA: KUZALIWA: 1974 KUFARIKI: 2013 UMRI: 39Yrs KANUMBA: Haya ni makazi ya milele ya Kanumba ambaye sasa ana mika 2 na miezi 2 KUZALIWA: 1984 KUFARIKI: 2012 UMRI: 28yrs Hakika vijana wengi hivi sasa wanaondoka duniani mapema mno, wakiwa na umri ch...

TUKIO ZIMA KATIKA PICHA: TAZAMA MAZISHI YA MSANII WA BONGO MOVIE RECHO, KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM.

Image
  Majeneza yenye miili ya Recho na mwanaye.   Miili ya Rachel Haule 'Recho' na mwanaye ikishushwa kwenye gari maalum baada ya kuwasili Viwanja vya Leaders ikitokea nyumbani Palestina, Dar tayari kwa kuagwa.   Waombolezaji wakiwa na simanzi baada ya mwili kuwasili Leaders.

WAZIRI DK. MUKANGARA AWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA HABARI , VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO BUNGENI

Image
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akiwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara yake kwa mwaka 2014/2015 mjini Dodoma jana. Waziri Mukangara ameomba Wizara yake iidhinishiwe kiasi cha Shilingi, 35,371,884,000 ambapo kati ya hizo jumla ya shilingi 20,371,884,000 ni za matumizi ya kawaida na kiasi kilichobaki ni fedha za miradi.  Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Habari wakifuatilia Hotuba hiyo.  Baadhi ya wadau wa Habari akiwepo Mkurugenzi wa Kituo cha Redio 5 cha jijini Arusha Francis Robert (kushoto) akifuatilia hotuba hiyo bungeni mjini dodoma leo.  Innocent Mungy kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akifuatilia mjadala wa Bajeti bungeni mjini Dodoma.  Wadau mbalimbali wa sanaa, Michezo na Utamaduni walikuwepo.  Wasanii wakifuatilia mjadala wa bajeti Bungeni, mtaalm Dude na kule P Funks mwaandaaji wa muziki na pia msaani wa muziki. ...

RECHO HAULE APUMZISHWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE, KINONDONI DAR

Image
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Nyerere akiweka shada la maua katika kaburi la Recho. Ndugu wa marehemu wakiweka mashada. Wasanii wa Bongo Muvi kutoka kushoto Aunt Lulu akiwa na wenzake. Watumishi wa Mungu (katikati) wakifanya maombi baada ya maziko. Mchumba wa marehemu George Saguda (kushoto) akiweka udongo katika kaburi la Rachel na mwanae. Msanii Blandina Chagula 'Johari' akiweka udongo kaburini. Mjomba wa marehemu, Evance Haule (kushoto) akiweka udongo katika kaburi la marehemu. Ndugu wa marehemu wakiweka mchanga katika kaburi la marehemu Rachel Haule. Mafundi wakichanganya zege. Mafundi wakisawazisha zege. (PICHA NA RICHARD BUKOS, DENIS MTIMA, MAYASA MARIWATA, SHANI RAMADHANI, HAMIDA HASSAN, IMELDA TARIMO/GPL)

MWILI WA RACHEL HAULE WAAGWA LEO HII, IRENE UWOYA AZIMIA. PICHA HIZI HAPA

Image
Mwili wa muigizaji wa filamu nchini Rachel Haule umeagwa leo hii katika viwanja vya Leaders na baada ya hapo atazikwa katika makaburi ya Kinondoni. Wasanii wengi ndugu, jamaa na marafiki wamejawa katika simanzi kubwa huku Irene Uwoya akizimia pengine kwa mshituko wa kuondokewa na msanii mwenzao. Angalia picha zikionyesha matukio ya mwili wa Rachel tangu akitolewa Muhimbili, kupelekwa Sinza na Leaders.......... Irene Uwoya akiwa amezimia 

Joseph Mbilinyi 'Sugu' Amlipua Zitto Kabwe

Image
Ni katika Hotuba yake ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo aliyoiwasilisha Bungeni leo hii muda mfupi uliopita. Waziri Kivuli Joseph Osmundi Mbilinyi aka Sugu amemtaja Zitto Z. Kabwe kama Mmiliki wa Kampuni ya Leka Dutigite aliyofanya biashara isivyo halali na Mashirika ya Umma ya NSSF na TANAPA.  Sehemu husika ya Hotuba hiyo ni hii: Mheshimiwa Spika, Tarehe 13 Agosti, 2012, Msajili Msaidizi wa Makampuni katika Wakala wa Usajili wa Makampuni na Leseni (BRELA) alitoa Hati ya Usajili (Certificate iof Incorporation) kwa kampuni inayoitwa Leka Dutigite Limited. Kwa mujibu wa nyaraka za BRELA, Leka Dutigite Ltd. ina ofisi zake katika ghorofa ya kwanza ya jengo la City House lililoko katika Mtaa wa Mkwepu, Dar es SalaaM. Mheshimiwa Spika,  Katiba, yaani Memorandum and Articles of Association, ya kampuni ya Leka Dutigite Ltd. iliyosajiliwa BRELA tarehe 13 Agosti, 2012 inaonyesha kwamba mwenye hisa nyingi katika ...