Posts

Showing posts from March 13, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN, MJINI DODOMA LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017. Picha na IKULU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017.

Waziri Ndalichako awaambia maofisa elimu kuhakikisha somo la Skauti linawekwa kwenye masomo ya ziada

Image
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amewataka maofisa elimu wa shule za msingi na sekondari nchini, kuhakikisha vyama vya skauti vinakuwa na masomo ya ziada katika shule hizo. Profesa Ndalichako aliyasema hayo hivi karibuni akiwa jijini Arusha kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, katika maadhimisho ya siku ya skauti Afrika ambayo kwa mwaka huu yalifanyika nchini. “Kama rais wa skauti na waziri mwenye dhamana ya elimu, naomba nitoe wito kwa maofisa elimu wote wa mikoa kuhakikisha suala la skauti shuleni linakuwa ni sehemu ya masomo ya ziada. Nasema hivyo kwa sababu mikoa mingine hapa washiriki ni wachache na nauliza kwanini tunawanyima vijana kushiriki kwenye mambo ambayo yana manufaa kwa Taifa,” alisema. “Tunataka wafanye nini, wakienda vijiweni hatuwaruhusu, hivyo tuwatengenezee mazingira na tutumie nguvu walizonazo katika mambo yatakayowajenga kuwa raia w

Zitto Kabwe ampongeza Kikwete kwa kuzindua taasisi yake ya maendeleo

Image
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete leo amezindua Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF).Taasisi hiyo imeundwa ili kusaidia Tanzania na Afrika katika kuimarisha amani, afya, utawala bora na maendeleo endelevu. Taasisi hiyo inajikita katika maendeleo endelevu kwa kusaidiana na wadau wengine kukabiliana na umaskini, kusaidia mkulima mdogo, kulinda mazingira na kukabiliana na athari za tabia nchi. Baada ya uzinduzi huo Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amempongeza Rais huyo mstaafu kupitia akaunti yake ya Facebook: “Hongera Sana Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuzindua Mfuko Wa Wakf Wa Jakaya Kikwete Foundation. Natumai utaitumikia vema nchi yetu na bara la Afrika katika ustaafu wako. Jambo moja kubwa uwekeze kwalo ni kuandaa Viongozi Vijana. Naona timu imesheheni watu wenye uwezo mkubwa. Kila la kheri.

HUYU NDIYE ALIYEMFUNDISHA OSAMA BIN LADEN UGAIDI

Image
Anaandika.Emanuel john. Ni Ali Mohamed alikuwa double agent wa CIA na EIJ( Egyptian islamic jihad) ambayo ndio ilipelekea kuundwa kwa ALQAEDA huku yeye akiwa mwendesha mafunzo wa mbinu za kivita na kijasusi wa kwanza kwenye kambi zao kwa ajili ya kuwaandaa na mapambano dhidi ya utawala wa kisovieti nchini Afghanistan miaka ya 90. yeye ndiye mwalimu wa kwanza wa Osama bin Laden na Ayman Zawahiry( kiongozi wa sasa wa Alqaeda) Ali anaelezwa kuwa mtu mwenye uzito wa kilo 90, urefu futi 6 huku akielezwa mtu aliye fiti kimwili, aliyebobea kwenye sanaa za mapigano( martial art),mwenye ufahasa mzuri wa lugha za kiingereza,kifaransa,kiyunani na kiarabu. alikuwa mwenye nidhamu ya juu, mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri, mwenye kujichanganya na watu na uwezo wa kupata marafiki kwa urahisi. Uhusiano wake na CIA kwa mara ya kwanza aliingia marekani kama mkalimani wa Ayman Zawahiry( kiongozi wa sasa wa alqaeda) wakati alipoenda kuchangisha michango kusaidia wana mgambo katika harakat

Hatimaye RC Paul Makonda aanza kazi tena leo hii baada ya kurejea toka Afrika ya Kusini

Image
Picha ikimuonyesha RC Makonda akizindua ujenzi wa barabara ya zege leo jijini Dar. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezindua Barabara ya Shimo la Udongo, Kilwa EPZ iliyopo Kurasini ya Umbali wa Kilomita 1. – Barabara hiyo iliyojengwa kwa kiwango cha zege na kampuni ya wazalendo ya Grant Tech imegharimu takribani milioni 350.

Msukuma afunguka mazito, Ni kuhusu alivyokamtwa na Polisi

Image
JOSEPH Kasheku “Msukuma” Mbunge waa Jimbo Geita Vijijini na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Geita ametoa siku tano za kuombwa na radhi na wanaodaiwa kuwa ni maofisa usalama wa Taifa waliotoa taarifa za uongo dhidi yake na kusababisha akamatwe Mjini Dodoma, anaandika Charles William. Juzi Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, liliwatia nguvuni Msukuma, Hussein Bashe, Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini na Adam Malima, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga kwa madai ya kupanga kufanya vurugu katika Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika jana. Wanasiasa hao walikamatwa na kuhojiwa, kabla ya kuachiwa kwa dhamana. Hata hivyo Msukuma amesema hawezi kukaa kimya juu ya suala hilo na kwamba wapo maofisa usalama waliosambaza taarifa juu yake na kusababisha hofu lazima wamuombe radhi. “Hawa ni wapiga dili, Rais lazima aiangalie upya Idara ya Usalama wa Taifa. Wameniundia mimi zengwe, mpaka nikakamatwa, na nchi ikawa kwenye presha, kama chama kisipozungum

KINANA AFUNGUA SEMINA ELEKEZI YA MABADILIKO NDANI YA CHAMA KWA WENYEKITI NA MAKATIBU WA CCM MJINI DODOMA LEO

Image
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifungua semina elekezi kuhusu mabadiliko ndani ya Chama, kwa Wenyeviti na Makatibu wa mikoa na wa wilaya na watendaji, leo katika Ukumbi wa Sekretarieti katika Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Katibu wa Sekretarieti ya CCM, Anamringi Macha (kulia) akiratibu semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani y

HIVI NDIVYO HALI ILIVYO JIJINI DAR LEO BAADA YA MVUA KUNYESHA

Image
 Kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa jijini Dar es salaam leo, soko la Sinza limelazimika kufungwa kwa muda kutoka na kujaa maji eneo lote la soko hilo.  Barabara nyingi za Dar leo zimejaa maji, hali inayopelekea magari mengi 'kubuma' kama ionekanavyo pichani hapa. Afande akitafakari jambo kufuatia uwingi wa maji katika barabara ya Bagamoyo eneo la Goigi jijiji Dar es salaam leo. Wadau wakifanya mambo katika moja ya chemba iliyoziba kutoka na wingi wa uchafu uliokuwa umesombwa na maji hayo.  Magari yote yamelazimika kupita upande mmoja wa barabara kutoka na wingi wa maji upande mwingine.