Miss Tanzania Diana Arushiana Maneno na Idrissa Sultani
Baada ya Idrisaa Sultani kumpiga vijembe Miss Tanzania 2o16 Diana Edward kukabidhiwa zawadi ya gari lenye mabango la lisilo na hadhi miss huyo amesema kuwa hawezi kumzuia kusema. Miss Diana alipewa gari aliloahidiwa kufuatia ushindi kwenye shindano lililofanyika October 2016, gari hilo limekuwa gumzo mitandaoni kutokana na mabango yaliyowekwa kwenye gari hilo. Kupitia Leo Tena ya Clouds FM leo May 12, 2017 Miss Tanzania 2016, Diana Edward amesema anatoa shukrani na anawaunga mkono waandaaji na hawezi kuwazuia watu kusema kwa kuwa hawafahamu namna gani wamepambana kulipata gari hilo. “Mabango yatatolewa siku hizi mbili na nimefundishwa kushukuru. Kwa hiyo, nilichopewa nimeshukuru. Nitaliendesha gari, sina kipingamizi. Maneno, watu watayaongea, hiyo ipo. Hakuna binadamu anayekubali kitu. Ndio uwezo wao ulipofikia wa kunipa hiyo zawadi. “Siwezi kuwapinga – ninawaunga mkono. Mimi ni binadamu pia, kwa hiyo, nimepewa zawadi na nimepokea kwa shukrani...