MSANII OTILIA LIVE NA ALLY YANGA
Richard Bukos, aliyekuwa Geita KATIKA hali iliyoashiria usaliti, Jumapili iliyopita msanii wa Bendi ya ToT, Otilia Boniface alinaswa ‘live’ na shabiki maarufu wa Yanga aitwaye Ally Said ‘Ally Yanga’ wakibusiana. Katika tukio hilo wawili hao walinaswa kwenye Viwanja vya Chato, mkoani Geita wakifanya usaliti huo huku Otilia na njemba huyo wakidaiwa kuziacha familia zao jijini Dar.Wakiwa kwenye starehe zao, paparazi wetu aliliona tukio hilo na kuanza kuwafotoa picha ambapo Ally Yanga aligeuka mbogo na kuanza kumchimbia mkwara paparazi wetu. “Ebwana mambo gani sasa hayo hebu futa picha hizo haraka sana tusije kuharibiana, mimi nina mke wangu naye ana mumewe hivyo hizo picha zitatuharibia,” alisema Ally Yanga. Akizungumza na paparazi wetu, Otilia alisema katika tukio hilo walikuwa wakisalimiana tu na hakukuwa na dhamira nyingine kwa kuwa kila mmoja ana ndoa yake. Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisikika akimtaja Ally Yanga kuwa ni mkali wa ‘totoz’ hivyo mume wa Otili...