Posts

Showing posts from June 24, 2016

PICHA 5: Muonekano wa helicopter inayotengenezwa Arusha

Image
Mtanzania Injinia Abdi Mjema ndiye anayeitengeneza helicopter hiyo katika chuo cha  ufundi Arusha na hadi kufikia mwezi wa saba mwanzoni itaanza majaribio ya awali, helicopter itakuwa na uwezo wa kuchukua abiria wawili na mpaka sasa shilingi million  3 zimeshatumika.

Kajala Akanusha Kutoka Kimapenzi na Msami

Image
Kajala na Msami Katika Pozi Msanii wa filamu Kajala Masanja amekanusha tetesi za kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatoka kimapenzi na mkali wa wimbo ‘Mabawa’, Msami. kajala Mwingizaji huyo ambaye hivi karibuni ilisambaa video inayomuonyesha akidendeka na rapa Quick Rocka, ameiambia Clouds Fm kuwa Msami ni mshkaji wake wa karibu sana na sio mpenzi wake. “Unajua kuna watu wanaweza wakawa labda ni washikaji au wana vitu vingi pembeni lakini watu wengine hawajui, mi na Msami ni washkaji sana,” alisema Kajala. Aliongeza, “Halafu sio kila siku watu watakuwa wanatuona barabarani au tunapostiana picha kwenye Instagram, lakini mimi na yeye tunaongea vitu vingi, kwa hiyo imekuwa rahisi mimi kuacha usingizi wangu kuja kwa Msami, sina uhusiano naye na vitu vingine mtavijua baadaye.” Wawili hayo wamekuwa wakioneka wakiwa pamoja mara nyingi hali ambayo imeibua hisia huenda wakawa wanatoka kimapenzi.

Wema Atoboa Siri Yake na Zari

Image
Wema Sepetu. Stori: Imelda Mtema, Ijumaa Dar es Salaam: Kwa mara ya kwanza, staa kiwango kunako sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ametoboa siri iliyofichika anayoijua mwenyewe kati yake na mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akieleza kuwa, hajawahi kumchukia wala kufikiria kumchukulia bwana’ke ila baadhi ya wapambe wake wamekuwa wakichochea kuwepo kwa bifu kati yao.   Zari. KISIKIE CHANZO Mmoja wa watu wa karibu wa mlimbwende huyo wa Tanzania mwaka 2006/07 aliyeomba jina lisichorwe gazetini aliling’ata sikio Ijumaa kuwa, Wema amekuwa akiumizwa na madai kuwa anamchukia Zari ‘Mama Tiffah’ wakati katika uhalisia siyo hivyo. “Wema amekuwa mgumu sana kumzungumzia Zari lakini safari hii ni kama uzalendo umemshinda kutokana na maneno ya watu hasa hili la kumzushia kuwa karudiana na Diamond. “Mwenyewe anasema hana tatizo na Zari ila hizi Timu Zari, Timu Diamond na Timu Wema ndizo zinachochea mam

BET Awards: Hizi ndizo baraka za Zari kwa Diamond

Image
Diamond Akiwa na Mpenzi wake Zari Hassan Hakuna baraka za muhimu kuzipata kama zile za mzazi wako na zile za mtu umpendaye. Kwa mwanaume baraka kutoka kwa mke wake zina nguvu mno hasa kwa kuwa maandiko matakatifu yanasema kuwa mwanamke alitokana na ubavu wa mwanaume. Mrs Nasib Abdul, Zari amempa baraka zake mpenzi wake Diamond ambaye amesafiri kwenda Los Angeles, Marekani kwenye tuzo za BET. Diamond ametajwa kuwania kipengele cha Best International Act: Africa. “Safari njema. May the Good Lord be with you all the way. Praying you bring the BET Award back to East Africa…. xoxo😍 @diamondplatnumz,” ameandika Zari kwenye Instagram. Hata hivyo kipengele hicho kina upinzani mkubwa mwaka huu. Msanii pekee ambaye ni tishio kwa Mond ni Wizkid. Staa huyo wa Nigeria mwaka huu amefanya mambo makubwa ikiwemo kushirikishwa na Drake kwenye wimbo ‘One Dance’ ulioshika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot 100 kwa wiki sita mfululizo. Pia amezunguka na Chris Brown kwenye zia

Hatma ya Uingereza Kujitoa Jumuiya ya Ulaya

Image
HISTORIA inaibeba Uingereza (England) ikijulikana kama moja ya nchi zenye nguvu zaidi duniani katika masuala ya kiuchumi na kijeshi.  Historia hii haipishani na ukweli halisi kwamba katika dunia ya sasa ya utandawazi  kila nchi inapigania kujijenga kiuchumi na ikihakikisha usalama wa uchumi wake na taifa kwa ujumla. Uingereza inabaki kuwa miongoni mwa mataifa yenye nguvu na ushawishi mkubwa katika masuala ya kimataifa ikijivunia historia yake, uchumi wake, nguvu yake ya kijeshi.  Hii ni pamoja  na nguvu kubwa ya ushawishi iliyonayo ikiungwa mkono na nchi nyingi za Amerika na Afrika. Kutokana na historia yake yenye kila aina ya ushawishi na kuogopwa,  ndivyo lilivyo kila jambo linalofanyika Uingereza ambapo huvutia macho na masikio ya watu wengi duniani vikiwamo vyombo vya habari kufuatilia na kuripoti kila jambo linalotokea kwa haraka. Inasemeka nguvu yake ya kihistoria na ushawishi wake kimataifa umeifanya ligi kuu yake ya mpira wa miguu maarufu kama English Premier

Uwoya Aitwa Ikulu ya Kenya

Image
                                                                 Irene Pancras Uwoya. IMELDA MTEMA, amani DAR ES SALAAM: Zali! Kuna madai kwamba, Rais wa Kenya, Uhuru Jomo Kenyatta amempa mwaliko maalum staa mwenye mvuto katika sinema za Bongo, Irene Pancras Uwoya kuitembelea ikulu ya nchini hiyo, ikiwa ni msanii wa kwanza Bongo kupata fursa hiyo, Amani limedokezwa. Kwa mujibu wa chanzo, awali rais huyo aliwahi kutolewa na jarida moja la nchini humo kwamba anazimikia sana kazi za filamu za staa huyo kutokana na filamu za Bongo Muvi. Rais wa Kenya, Uhuru Jomo Kenyatta ATUMA WATU KUJA BONGO Mpashaji wetu huyo alizidi kufunguka kuwa, Rais Uhuru aliwatuma wasaidizi wake kuja Bongo kumsaka staa huyo ambapo walipata maelekezo sahihi mpaka wakafika  nyumbani kwa wazazi wake,  Mbezi Beach jijini, Dar ambako walipata maelekezo sahihi ya kumpata Uwoya mwenyewe. UJUMBE WAKUTANA USO KWA USO NA UWOYA “Baada ya kuelekezwa jinsi ya kumpata Uwoya, walifunga safari mpaka Sin

David Cameron Ajiuzulu

Image
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron ametangaza kujiuzulu wadhifa huo baada ya Uingereza kupiga kura ya kujitoa rasmi kwenye Umoja wa Ulaya (EU). Cameron ametangaza uamuzi huo wakati akitoa hotuba yake ambapo amesema Uingereza inahitaji uongozi mpya. Itachukua miezi mitatu kuandaa serikali ijayo. Wakati hayo yakitokea, Paundi ya Uingereza yaanguka dhidi ya dola ya Marekani baada ya kura ya kujitoa EU, anguko hilo halijapata kutokea tangu mwaka 1985. Matokeo yaonesha asilimia 52% ya Waingereza wamepiga kura kutaka kujitoa katika Umoja wa Ulaya huku 48% wakitaka kubaki katika umoja huo

RAIS DKT. MAGUFULI AKABIDHIWA REPOTI YA UCHAGUZI MKUU WA 2015.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali mara baada ya kupokea Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Damian Lubuva Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Damian Lubuva Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha UDP mzee John Momose Cheyo mara baada ya kumaliza kuzungumza na wageni mbalimbali katika tukio la upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Fahmi Dovutwa mara baada ya kuhutubia katika tukio la upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Rais wa Jamh