Wema Sepetu azimia mara tatu kufuatia kifo cha baba yake mzazi, balozi Abraham Isaac Sepetu
Wema Sepetu amabaye ni Miss Tanzania 2006 na pia muigizaji wa filamu Tanzania amezimia mara tatu ndani ya masaa saba juzi kufuatia kupata msiba wa baba yake mzazi balozi Abraham Isaac Sepetu ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za juu katika serikali ya Tanzania. Wema alipatwa na hali hiyo baada ya kutoamini kuwa hatamuona tena baba yake mzazi ambaye alikuwa anampenda sana. Chanzo kimoja kikizungumza na GPL kilisema: "Wema bado mdogo, katika maisha yake hakuwahi kupatwa na msiba mkubwa kama huu, kumpoteza baba yake kipenzi, ni jambo zito ndiyo maana mpaka sasa tunapoongea ameshazimia mara tatu, yaani anazimia na kurejewa na fahamu." Jumapili saa 7 mchana baada ya kurejewa na fahamu, Wema Sepetu alifunguka na kuelezea uchungu wa kumpoteza baba yake mzazi akidai kuwa kifo hicho ni pigo kubwa maishani mwake ambalo hakuwahi kulifikiria. "Nimeumia sana kwani huu ni msiba mkubwa kwangu, Baba yangu alikuwa nguzo imara ...