Posts

Showing posts from April 5, 2018

Mtanzania Mahakamani Uingereza Akidaiwa Kumuua Mkewe

Image
Raia wa Tanzania Kema Salum. RAIA wa Tanzania Kema Salum (38) amefikishwa mahakamani nchini Uingereza akidaiwa kumuua mkewe, Mtanzania pia, aitwaye Leyla Mtumwa. Salum anayedaiwa kumchoma visu Leyla na kumuua wakiwa nyumbani kwao mtaa wa Kirkstall, Haringey, nchini humo Ijumaa iliyopita, amefikishwa katika mahakama ya Crown. Marehemu Leyla Mtumwa. Kutokana na mgomo wa wanasheria nchini humo tangu kuanza kwa mwezi Aprili, kesi hiyo haikusikilizwa na Jaji Anuja Dhir ameahirisha usikilizwaji wake hadi Juni 20 mwaka huu. Kwa mujibu wa mwanasheria Seona White, juhudi zinafanyika ili kupata wakili wa kumtetea Salum mahakamani licha ya mgomo wa mawakili unaoendelea. Mtuhumiwa huyo alisomewa mashitaka yake kwa Kiingereza lakini kupitia mkalimani aliyemwelewesha kwa Kiswahili. Mipango inafanywa kumleta marehemu nchini Tanzania.

JPM Awalilia 12 Waliokufa Ajalini Tabora, Ataka Polisi Kujitathmini

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 12 vilivyotokea katika ajali ya basi kugongana na lori Kijiji cha Makomero, Wilaya Igunga mkoani Taborausiku wa kuamkia leo.

Hatma ya Nabii Tito aprili 13

Image
KESI  inayomkabili Tito Machibya maarufu Nabii Tito, hatma yake kujulikana Aprili 13 mwaka huu baada ya mahakama ya Wilaya ya Dodoma kupokea taarifa za kitabibu jana asubuhi. Mahakama ya Wilaya ya Dodoma jana ilipokea taarifa ya vipimo vya kitabibu vya Tito Machibya, ilivyokuwa imeviagiza hapo awali na kumtaka afanyiwe vipimo katika Taasisi ya magonjwa ya akili ya Isanga mjini Dodoma. Jana Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha alisema mahakamani hapo kuwa alipokea taarifa ya kitabibu kuhusu Nabii Tito kutoka Taasisi ya Isanga hivyo ataipitia na kutoa maamuzi siku hiyo ya Aprili 13. “Nieleze kuwa nimepokea taarifa ya kitabibu kuhusu mtuhumiwa huyu leo asubuhi hivyo nitaipitia ili April 13 mwaka huu siku ya Ijumaa niweze kuitolea maamuzi,” alisema Karayemaha. Hata hivyo Nabii Tito jana aliweza kuhudhuria mahakamani akitokea mahabusu ya gereza kuu la Isanga baada ya kutofikishwa mahakamani  hapo  mara mbili mfululi...

Mbasha afunguka ishu ya kumpa mimba Agness

Image
Msanii wa nyimbo za Injili nchini, Emmanuel Mbasha amesema amesikitishwa na taarifa alizozipata kuwa amempa ujauzito msichana anayevuma kwenye mitandao ya kijamii Agness na kudai hana mahusiano yeyote na mtu huyo zaidi ya kumfahamu kupitia mitandaoni. Mbasha amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana baada ya kuwepo na tetesi za muda mrefu zinazozidi kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa zinadai kuwa wawili hao wana mahusiano ya kimapenzi na mpaka kufikia hatua ya kukubalia kupeana ujauzito. "Agness mimi namfahamu kama shabiki yangu kupitia mitandao ya kijamii. Sasa sielewi mambo yamegeuka vipi mpaka kufikia hatua ya kuambiwa mimi nina mahusiano naye. Sijawahi kuwa na mahusiano na Agness na wala sijawahi kuwa na chochote kile kinachoashiria mapenzi", amesema Mbasha. Pamoja na hayo, Mbasa ameendelea kwa kusema "sitegemei kupata naye mtot...

Ndugai: Bashe Apeleke Hoja Yake Kwenye Chama Kabla ya Bungeni

Image
Bashe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yustino Ndugai amesema suala la Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe kutoa hoja binafsi bungeni, alitakiwa kuipeleka kwenye chama chake kwa ajili ya kujadiliwa kabla ya kuipeleka bungeni. Ndugai amesema hayo ikiwa ni siku chache baada ya kurejea kutoka India alikokuwa akipatiwa matibabu. Amesema Kanuni za Bunge zipo na Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Bunge kwa wabunge wa CCM kama chama tawala na zipo, kama kwa wabunge wa kambi ya upinzani ambazo zote ni sehemu ya uendeshaji wa shughuli za Bunge. Ndugai. Amesema Bashe kama mbunge wa CCM, kanuni za wabunge wa CCM zinamtaka aipeleke hoja yake kwenye chama chake kwanza, ikajadiliwe huko na ikikubaliwa Bunge liweze kuipokea. Amesema Bunge bado halijapokea hoja hiyo kutoka kwa Bashe, pia halijapokea taarifa kutoka kwa katibu wa wabunge wa CCM kama wameipokea hoja hiyo na wameshaurianaje. Mwezi uliopita, Bashe alisema amemuandikia barua...

Watu wanne wadakwa kwa tuhuma za wizi katika Ujenzi wa reli ya kisasa

Image
Watu wanne wanashikiliwa na Polisi Ngerengere, Mkoani Morogoro wakituhumiwa kuhusika na wizi wa lita 2510 za mafuta aina ya Dizeli kutoka kambi ya ujenzi wa reli ya kisasa Standard Geuge. Watuhumiwa hao wamekamatwa na polisi kikosi maalumu cha reli nchini kwa kushirikiana na maafisa wa shirika la reli Tanzania ambapo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika. Akizungumza na waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Kikosi Maalumu cha Reli Salum Kisai, amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao itakuwa fundisho kwa watanzania wengine wanaofanya kazi katika mradi huo ili kuweza kulinda mali za mkandarasi na kumaliza kwa mradi huo kwa muda unaotakiwa. Kwa upande wake Afisa wa shirika la Reli nchini TRC Catherine Mushi, amesema wananchi wanapaswa kushiriki katika kulinda miundo mbinu ya reli hiyo ikiwa ni pamoja na kuongeza uaminifu kwa wawekezaji nchini kuweza kutoa ajira zaidi kwa watanzania.