Posts

Showing posts from December 27, 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI LINDI KWA ZIARA YA KIKAZI KATIKA WILAYA YA RUANGWA

Image
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Lindi Godfrey Zambi mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea kwa ajili ya ziara ya kikazi katika wilaya ya Ruangwa Mkoani lindi kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi  Alli Mohamed Mtopa  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi wa Nachingwea (DED) Bakari Mohamedi Bakari katika kiwanja cha ndege cha Nachingwea wakati wa mapokezi ya waziri mkuu wilayani hapo waziri mkuu amefika kwa ziara ya kikazi katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi  Waziri mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mery Majaliwa wakifurahia ngoma ya kikosi cha JKT  843KJ kilichopo Nachingwea ambacho kilikuwepo katika mapokezi ya Waziri Mkuu katika uwanja wa ndege wa Nachingwea .Picha na Chris Mfinanga

MWANAFUNZI ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUKATWA MAPANGA NA MWALIMU

Image
MWANAFUNZI Marco Limbe(14) aliyemaliza darasa la saba mwaka huu katika shule ya msingi Yitwimila iliyoko kata ya kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu amelazwa katika kituo cha afya Busega mara baada ya kuchalangwa mapanga kichwani na mdomoni na mwalimu wake. Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.30 jioni wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akirejea nyumbani kwao akitokea katika malisho ya mifugo ndipo alipokaribia katika shamba la mwalimu Pendo Gabriel ndipo mwalimu huyo alimkamata kijana huyo na kuanza kumchalanga kwa panga na kupelekea kijana limbe kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 mara baada ya kufikishwa katika kituo cha afya Busega. “Shuhuda wa tulio hilo aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Manoga anaeleza kuwa ilikuwa kama mchezo lakini kumbe ni kweli kwani niliona mifugo ya limbe iliyokuwa ikielekea nyumbani na huku limbe akiwa nyuma ya mifugo hiyo katika barabara ambalo liko karibu na maeneo ya shule ghafla nilimuona mwalimu pendo w...

MANENO YA ZITTO BAADA YA KUPATA MTOTO WA KIKE

Image
July 14, 2016  Mbunge wa Kigoma mjini,  Zitto Kabwe  aliingia kwenye headlines za kuuacha rasmi ukapera baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake.  Good news leo December 27 2016 Zitto Kabwe na mkewe wamepata mtoto wa kike ambaye wamempa jina la Josina – Umm Kulthum. Zitto Kabwe amezitoa taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii na amesema kuwa wamempa jina hilo kwa heshima ya mwanamama mpigania uhuru wa Kusini mwa Afrika, Josina Muthembi Machel wa FRELIMO, aidha amesema Umm Kulthum kwa heshima ya mama yake mdogo na pia jina la binti wa Mtume Muhammad (SAW).

MAGAZETI YA LEOJUMANNE TAREHE 27.12.2017

Image
 

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image