Posts

Showing posts from March 1, 2018

Shilole Ahukumiwa kwa Utapeli, Mahakama Kukamata Mali Zake!

Image
Shilole akiwasili mahamani hapo. MSANII wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 14 na mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kupatikana na hatia ya utapeli kusababisha hasara kwa kushindwa kufika kwenye shoo. …Akiwa na mumewe Uchebe. Katika kesi hiyo iliyotolewa hukumu leo Machi 1, 2018, imethibitika kuwa Shilole alilipwa kiasi cha Tsh. Milioni tatu kwa Mary Musa kwa ajili ya kutumbuiza siku ya mkesha wa Pasaka mwaka jana 2017 katika Ukumbi wa Heineken uliopo Mbagala-Kijichi jijini Dar es Salaam lakini alishindwa kutokea kwenye shoo hiyo kama walivyokubaliana. …Akiingia ndani ya chumba cha mahakama. Kutokana na kitendo hicho,  mashabiki waliofika kwenye shoo hiyo walipandwa hasira na kufanya fujo huku wakiharibu mali ukumbini hapo hivyo kumsababishia mwandaaji ambaye ni Mary, hasara ya Tsh. Milioni 14 ambazo mahakama imeamua Shilole azilipe kama fidia kwa mlalamikaji. Mlalamika...

Wimbo wa Kibamia wamponza Roma Mkatoliki, afungiwa miezi sita

Image
 Msanii Roma Mkatoliki  Msanii wa Bongo Fleva, Roma Mkatoliki amefungiwa miezi sita kutojihusisha na Muziki ikiwa ni kutekeleza azma ya Serikali kwa kile kinachodaiwa kukiuka maadili ya jamii za kitanzania kwenye wimbo wake wa "KIBAMIA". Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, amesema kuwa Roma amedharau wito wa serikali ambapo leo aliitwa ili ahojiwe   kutokana na wimbo wake huo ikiwa ni hatua ya pili mara baada ya Baraza la Sanaa Nchini Basata kumuita na kumtaka arekebishe baadhi ya sehemu katika wimbo huo. "Tumempigia simu mara kadhaa hajapokea, tumemtumia meseji anasoma lakini hajibu chochote hivyo hiyo ni dharau na hatuendelei kudili na mtu mmoja wasanii ni wengi ambao wanahitaji msaada kutoka kwetu" alisema Shonza.

Rais Shein aongeza Wizara, Apangua Baraza la Mawaziri

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko katika Baraza la Mapinduzi huku akiongeza wizara moja zaidi. Kwa mujibu wa taarifa Ikulu ya Zanzibar, shughuli za Vijana zimehamishiwa katika wizara mpya ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo; shughli za Mazingira zimehamishiwa katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais huku shughli za Wakala wa Serikali wa Uchapaji zimehamishiwa Wizara mpya ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale. Mabadiliko hayo yanaifanya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa na Wizara 14 zenye Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo: 1. OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI i. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi- Issa Haji Ussi Gavu 2. OFISI YA RAIS, KATIBA SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NAUTAWALA BORA i. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora –Haroun Ali S...

Breaking News: Mlipuko Watokea Mahakama Ya Kisutu

Image
Muonekano mahakama ya Kisutu baada ya kutokea mlipuko uliosababishwa na umeme. Mahakama ya Kisutu imekumbwa na hitilafu ya umeme leo baada ya mvua kunyesha na kusababisha mlipuko na sintofahamu mahakamani hapo. Hitilafu hiyo ya umeme inadaiwa kutokea kwenye moja ya vyumba katika mahakama hiyo.

CDF Mabeyo Awatahadharisha Watanzania

Image
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo amewahadharisha Watanzania na kuwataka wajiepushe na vitendo vinavyoweza kutishia usalama wa nchi na kuharibu tunu ya amani iliyopo. Ameeleza kuwa hivi sasa vipo viashiria vinavyotishia usalama wa nchi, na kwamba hatua zinachukuliwa ili kudhibiti hali hiyo. Jenerali Mabeyo amewaomba Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli dhidi ya wizi, ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi za umma, kwa kuwataja hadharani watu wanaojihusisha na vitendo hivyo Mabeyo amesema vita dhidi ya wizi na ufisadi, iliyoanzishwa na Rais Magufuli, si ya mtu mmoja, bali kila Mtanzania anapaswa kushiriki, kwani mali zinazoibwa na baadhi ya Watanzania, zinapaswa kuwanufaisha watu wote.

Hii ndio Mikoa vinara wa vifo vinavyosababishwa na wivu wa mapenzi

Image
Mikoa ya Singida na Tabora imebainika kuwa vinara wa matukio ya mauaji baina ya wanandoa katika miaka ya 2016 na 2017, kwa kuwa na matukio 314 kutokana na wivu wa mapenzi na ugomvi wa kifamilia. Takwimu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kupitia Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Barnabas Mwakalukwa kwa gazeti la Habari Leo, zinaonesha kuwa, mwaka 2016 kulikuwa na mauaji 151 baina ya wanandoa. Mwaka 2017 mauaji hayo yaliongezeka na kufikia 163 ambayo ni nyongeza ya mauaji 12 sawa na asilimia 7.9. Zinasema Mkoa wa Singida ulikuwa na matukio 27 ukifuatiwa na Tabora uliokuwa na mauaji 26 baina ya wanandoa. Mikoa mingine iliyofuata kwa wingi wa matukio ya wanandoa kuua wenza wao na idadi kwenye mabano ni Geita (25), Mwanza (21), Kagera (20) Mbeya 19 na Shinyanga (18). Mwaka 2016 Mkoa wa Shinyanga uliongoza kwa wanawake saba kuua waume zao, ukifuatiwa na Tabora sita huku mikoa ya Singida na Iringa ikiwa ...

Matukio Mabaya, Yawaongoze Kufanya Maamuzi Magumu!

Image
N I vigumu sana kumuacha mtu umpendaye. Unapompenda mtu mara nyingi hufikirii kufanya maamuzi yoyote hasi. Akili yako kamwe haimuwazii mambo mabaya mwenzi wako. Matamanio ya moyo wako ni kuona mnazidi kupendana. Mnazidi kuweka upendo mbele katika kila jambo linalowatokea katika maisha yenu. Upendo unawafanya muwe kitu kimoja katika maamuzi. Upendo unawapa faraja katika maisha yenu. Upendo unawafanya mchukuliane kwa kila hali, mathalani masuala ya ugonjwa na matatizo mengine. Shida yako ni shida yake, ya kwake pia inakuwa yako. Upendo unapowazunguka wapendanao wanakuwa wanaishi katika ulimwengu wao. Mkiishi katika misingi ya upendo, ni nadra sana kuona ugomvi kwa wapendanao. Pamoja na hayo, kuna wakati huwa yanatokea matatizo mbalimbali katika uhusiano ambayo kimsingi wakati mwingine yanapoteza ladha ya uhusiano. Hii inaweza kujidhihirisha kipindi tu mnaanza uhusiano, wakati mwingine huwa inatokea mkiwa tayari kwenye kilele cha safari yenu. Mfano inawez...