Posts

Showing posts from April 9, 2017

MBUNGE WA JIMBO LA MTAMA MH. NAPE NNAUYE AZUNGUMZA NA WAZEE

Image
Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akiwasili katika kikao cha kati yake na wazee wa Mtama kikilchofanyika kwenye ukumbi wa kanisa katoliki kijiji cha Majengo A huku akiwa ameongozana na Katibu Msaidizi wa Wilaya ya Lindi Vijijini Bw. Shaibu Bakari Ngatiche Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya wazee wakati alipowasili katika ukumbi wa mkutano wake kati ya yake na wazee Mtama. Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akizungumza na wazee wa Mtama leo kwenye ukumbi wa kianisa Katoliki Kijiji cha Majengo A. Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akifurahia jambo wakati akizungumza na wazee hao leo. Baadhi ya wazee wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Mtama Mh. Nape Nnauye wakati akizungumzza nao leo. Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lindi vijijini Bw. Mohamed Nanyali akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wakati akimkaribisha Mbunge wa jimbo hilo Mh. Nape nnauye ili kuzungumza na wapiga kura wake.

ABIRIA AJIFUNGUA MTOTO NDANI YA NDEGE FUTI 42,000 ANGANI

Image
Haki miliki ya pichaTURKISH AIRLINES Wahudumu wa shirika la ndege la Uturuki wakiwa na mtoto aliyezaliwa Wahudumua wa ndege ya shirika la ndege la Uturuki, walisherehekea kuwasili kwa abiria mwingine angani umbali ya futi 42,000 au mita 12,800, wakati mwanamke mmoja alijifungua mtoto msichana. Abiria nao walisaidia kuzaliwa kwa mtoto huyo, muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka mji mkuu wa Guinea, Conakry, ikielekea Isanbul kupitia Burkina Faso. Mama wa mtoto huyo aliyepewa jina Kadiju, walipelekwa hospitali wakati ndege hiyo aina ya Boeng 737 ilipotua mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou. Haki miliki ya pichaTURKISH AIRLINESI Abiria ajifungua mtoto ndani ya ndege angani Haki miliki ya pichaTURKISH AIRLINES  Abiria ajifungua mtoto ndani ya ndege angani Wote waliripotiwa kuchoka lakini walikuwa na afya nzuri. Wahudumu waligundua kuwa mwanamke mmoja abiria kwa jina Nafi Diaby, alikuwa akihisi uchungu wa kujifungua. Hapo ndipo walichukua hatua ya kumsaid...

ALICHOSEMA ROMA MKATOLIKI BAADA YA KURUHUSIWA KUTOKA POLISI

Image
Tangu zilipotoka taarifa kuwa ROMA Mkatoliki na wenzake watatu waliokuwa wamekamatwa na watu wasiojulikana wamepatikana wakiwa wazima Watanzania wengi wamekuwa na shauku ya kujua ni jambo gani kina ROMA wanaweza kuzungumza kuhusu tukio hilo. Baada ya kuruhusiwa na Polisi, ROMA amezungumza kwa ufupi kuhusu tukio hilo lakini akiwa hayupo tayari kuelezea kwa undani hadi pale watakaporuhusiwa na Polisi kwani kwa sasa taratibu za kiusalama haziwaruhusu kuelezea ni nini kimetokea.“Kwa kifupi tu niwahakikishe mimi ni mzima niko vema kabisa kiafya, kiakili na vinginevyo na hata wenzangu watatu nikimaanisha Mona, Bin Laden pamoja na Imma, tunaendelea vizuri na kwa sasa tupo katika taratibu za kutoa taarifa ya tukio zima, taratibu hizo zinatufunga tusiongee chochote kwa sasa hivi, “Ratiba ninayoweza kuwapa kupita kesho jumapili, siku ya jumatatu nadhani kutakuwa na press conference ya kuelezea habari nzima ilikuwaje, nawashukuru Watanzania wote sijapata nafasi ya kuingia ...

MZEE NDESAMBURO ALIVYOIPASUA CHADEMA KASKAZINI

Image
Wiki iliyopita kulikuwa na uchaguzi ndani ya Chadema ulilenga kuwapata viongozi wa Kanda ya Kaskazini lakini ukahirishwa ghafla na siku ya mwisho. Kuahirishwa kwa huo, licha ya kunaonekana kama ni tukio la kawaida kulizingira na mambo mengi yaliyojificha nyuma ya pazia. Chadema imekuwa ikiendelea na mipango yake ya kupanga safu za uongozi kwa kuzingatia sera yake ya kugatua madaraka ya chama kitaifa kwa ngazi za Kanda na wiki iliyopita ilikuwa zamu ya Kanda ya Kaskazini – yaani mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga ambako uchaguzi huo ulikuwa ufanyike. Uchaguzi huo kulingana na vyanzo mbalimbali ndani ya chama hicho uliahirishwa kutokana na mvutano ulioibuka ndani ya Kamati Kuu ya Chadema iliyoketi Tanga, baada ya kuwapo shinikizo la kutaka mwenyekiti wa Chadema Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo asigombee nafasi ya mwenyekiti wa Kanda. Ndesamburo ambaye amekuwa mbunge wa Jimbo la Moshi mjini (2000-2015) alipoamua kutogombea, aliamua kuwania nafas...