Posts

Showing posts from January 18, 2016

DIAMOND PLATINUMZ ANA MTOTO MWINGINE MWANZA ....AELEZA STORY NZIMA SOMA HAPA

Image
Tiffah Dangote ana ndugu yake, aliyezaliwa na msichana aliyekutana kimapenzi na baba yake (one night stand), Diamond Platnumz enzi anaanza kuupata ustaa. Taarifa hizo zilitolewa hivi karibuni na Diamond mwenyewe wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Papaso cha TBC FM. Anasema tukio hilo lilitokea mwaka 2010, Mwanza alikoenda kufanya show. “Huyo mwanamke story ilivyokuwa alikuwa ametoka kwenye chumba cha brother Dully akaja kwangu mimi nikafanya yangu, mimi nikarudi huku mtoto akawa ananimbia ‘ebwana mimi nina mimba,” alisimulia Diamond. “Basi ilivyokuwa mtoto ‘bana eeh mimi nina mimba’ na mimi nikawa nachezesha nini nikawa namhudumia, huku na huku bahati mbaya nikaanza na demu fulani hivi kwahiyo demu mwenyewe akanimind, nikawa nampigia simu hapokei nikaenda Mwanza kumsakanya huku na huhu nasikia kwao wakanimind nikaonekana kama mimi nazingua,”alisema. “Siku moja nikaenda nikambanabana ‘nikamwambia wewe una mtoto’ akanikatalia kwasababu aliniambia ile mimba n

Mkurugenzi Mamlaka ya Viwanja vya Ndege afariki dunia

Image
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Said enzi za uhai wake. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Said amefariki dunia mapema leo asubuhi akiwa katika mazoezi ya kuogelea,taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Bwa.Suleiman alikimbizwa hospitali ya Agakhan kwa matibabu, na baadae ikaelezwa kuwa amekwisha fariki na kuwa mazishi yanatarajiwa kufanyika leo.

Waziri Mkuu amwakilisha Rais Magufuli mkutano wa SADC Gaborone

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Botswana, Bw. Tshenolo Mabeo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama uliopo Gaborone Januari 17, 2016. Majaliwa amemwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa SADC. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mtendaji wa SADC,Dkt, Srergomena Tax mjini Gaborone ambako Mheshimiwa Majaliwa anamwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa SADC Januari 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BREAKING NEWS : WANANCHI WA BONDE LA MKWAJUNI WAFUNGA BARABARA NA KUFANYA FUJO

Image
Hali si shwari hivi sasa katika eneo la Bonde la Mkwajuni Kinondoni jijini Dar es salaam, na inaelezwa kuwa baadhi ya Wananchi wamechoma mataili pande zote za barabara na hakuna gari kupita. Jeshi la Polisi lipo eneo la tukio hivi sasa kukabiliana na tukio hilo ambalo chanzo chake unadaiwa ni baadhi ya vijana wanaodaiwa kuwa walikuwa wakazi wa eneo lililobomolewa ambao wameingia barabarani na kufanya fujo. Pia gari la zimamoto limefika eneo la tukio ili kuzima moto huo. (Picha zote na Henry Mdimu) Endelea kutufuatilia kwa habari zaidi.  

Wakurugenzi watendaji Manispaa za Kigoma, Mpanda wasimamishwa

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhe. George B. Simbachawene. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhe. George B. Simbachawene amewasimamisha kazi wakurugenzi watendaji wa manispaa za Kigoma, mkoa wa Kigoma na manispaa ya Mpanda, mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kuridhia na kutekeleza maamuzi ambayo yamesababishia serikali hasara na upotevu wa fedha. Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma, Mhandisi Boniface Nyambele anakabiliwa na tuhuma ya uuzaji wa nyumba za halmashauri bila kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo na bila kibali cha waziri mwenye dhamana kama sheria inavyoelekeza. Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda, Ndugu Suleiman Lukanga anakabiliwa na tuhuma za ununuzi hewa wa gari la kusomba taka kwa kiasi cha shilingi milioni tisini na mbili, laki saba na elfu hamsini (92,750,000/=) na ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa skimu ya umwagiliaji ya Kakese kiasi cha shilingi milioni mia m