ZITTO KABWE AWAPONDA LOWASSA NA MAGUFULI
Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe. Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema hakuna tofauti kati ya mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa aliyechukua fomu ya kugombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokana na wote kutokuwa na ubavu wa kupambana na ufisadi. Zitto alisema hayo jana katika mkutano mkuu wa ACT- Wazalendo Jimbo la Kigoma Mjini, uliokuwa maalum kwa ajili ya kupiga kura ya maoni ili kupata mgombea wa ubunge wa chama hicho Jimbo la Kigoma Mjini. Alisema katika mazingira ya sasa ya kisiasa nchini, ni ACT-Wazalendo pekee ambacho kinaweza kusimama na kusema kinapambana na ufisadi. Alisema kutokana na chama hicho kuchukia rushwa ndiyo maana kimetoa msimamo kuwa hakiwezi kushirikiana na chama chochote ambacho maadili ya viongozi wake yanatia shaka. Zitto alisema uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakuwa mgumu na ushindani m...