Taarifa mpya ya Wizara ya Habari na sanaa kuhusu Roma kutoweka
Taarifa za kupotea kwa Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wawili baada ya kutekwa na kuchukuliwa na Watu wasiojulikana kwenye studio za TONGWE Dar es salaam, zilianza kusambaa kuanzia juzi usiku (April 5 2017) Leo April 7 2017 Wizara ya Sanaa, Utamaduni na michezo ambayo iko chini ya Dr. Mwakyembe imetoa taarifa ifuatayo >>>> “kwa dhamana yake katika tasnia ya Sanaa Wizara imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki Ibrahim Mussa kwa jina la kisanii “Roma Mkatoliki”” Wizara imefuatilia kwa karibu suala hili kwa kuwa lina muelekeo wa jinai. Hata hivyo taarifa kutoka vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi. Kutokana na hali hiyo, Wizara inawaomba wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zozote zitakazo saidia kujua alipo msanii huyo.