Posts

Showing posts from June 18, 2018

Mshambuliaji wa Croatia atimuliwa Urusi, kisa kukataa kuivaa Nigeria

Image
Mshambuliaji timu ya taifa ya Croatia Nikola Kalinic amerudishwa nyumbani baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu. Kocha wake, Zlatko Dalic alimtaka mshambuliaji huyo kuingia katika dakika za mwisho katika mechi yao dhidi ya Nigeria, akagoma. Kalinic aligoma akidai alikuwa na maumivu ya mgongo. Hivyo akakataa kuinuka na kuingia kama kocha huyo alivyotaka. Pamoja na kwamba aliomba msamaha baada ya Croatia kushinda kwa mabao 2-0 katika mechi hiyo, Dalic alikataa katakata na kusisitiza, arejee nyumbani Croatia.

CHIDI BENZ ANASWA NA MZIGO WA BANGI DODOMA

Image
STAA wa Bongo Fleva, Rashidi Makwiro maarufu kama ‘Chid Benz’ amekamtwa na Jeshi la Polisi jijini Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na mzigo wa bangi kiasi cha gramu tano. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema hayo leo Jumatatu, Juni 18, 2018 wakati akizungumza na wanahabari jijini humo baada ya kumtia mbaroni msanii huyo.   Hii ni mara ya pili kwa Chidi kukamatwa na madawa ya kulevya mwaka huu mkoani Dodoma huku akidai kuwa alishaacha kutumia madawa hayo na anaendelea na matibabu Sober House. Hii ni sehemu ya taarifa ya polisi kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa mbaliombali akiwemo Chidi.

Mbowe Apata Pigo, Aanguka Ghafla, Akimbizwa Muhimbili

Image
MWENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuanguka ghafla alfajiri ya leo Jumatatu, Juni 18, 2018, hii ni kwa mujibu wa wakili wake Jeremiah Mtobesya. Wakili Mtobesya, aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa mteja wake alianguka leo akiwa nyumbani kwake, hivyo asingeweza kufika mahakamani kwa siku ya leo. Akiwasilisha taarifa hiyo, Wakili Mtobesya ameeleza kuwa Mbowe ambaye ni mshtakiwa namba moja katika kesi namba 112 ya 2018 amefiwa na kaka yake Henry Mbowe usiku wa kuamkia leo. Naye Msemaji wa Chadema, Makene amesema; “Ni kweli Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mh. Freeman Mbowe amepatwa na shida ya kiafya asubuhi ya leo akiwa nyumbani kwake, na amelazwa Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Dharura. Tutaenelea kuwajuza.” Aidha, awali Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliiambia mahakama kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya washtakiwa Mbowe na wenzake w...

BREAKING: BAJETI YA UPINZANI YAZUIWA BUNGENI, WENYEWE WASUSA

Image
#GLOBALHABARI: Hotuba ya Bajeti mbadala ya Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imekataliwa bungeni kutokana na kuwasilishwa nje ya utaratibu. Wabunge wa upinzani (isipokuwa wanaomuunga mkono Prof Lipumba ) wameondoka kwenye ukumbi wa Bunge.