HII STORI YA MAISHA YA MWIGIZAJI MASANJA INAWEZA KUKUTOA MACHOZI
Masanja Mkandamizaji si jina geni masikioni mwa watu wengi kutokana na uwezo wake wa kuwavunja mbavu watazamaji pale anapoonekana katika runinga na Kundi la Original Comedy. Licha ya kufika hapo alipo sasa, anakiri wazi kuwa amepitia katika maisha magumu hususani wakati alipoamua kuanza maisha binafsi ya kujitegemea baada ya kutoka nyumbani kwa dada yake alipokuwa akiishi. Anasema kabla ya kuondoka kwa dada yake alimuomba amtafutie chumba ili ajitegemea na kuanza maisha binafsi kama kijana . Nilimwambia dada anitafutie chumba na alifanya hivyo ingawa alikuwa anahofia kama nitaweza ,basi nikapata 'geto' langu maeneo ya Tabata Aroma na nilitakiwa kulipa kodi ya TSh. 5,000 kwa mwezi, anasema Masanja. Anakiri wazi kuwa changamoto katika maisha ndizo zilizochangia kumfikisha mahali alipo sasa kwani licha ya kuwa katika hali ngumu Hakukata tamaa bali alizidi kujituma kwa nguvu zake zote. Anasema kuna wakati ilikuwa vigumu kuipata hata hiyo hela ya kodi kwahiy...