Posts

Showing posts from April 25, 2016

Maajabu Mazishi ya Liyumba

Image
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Joachim Liyumba enzi za uhai wake. Stori: Dustan Shekidele, Wikienda MAHENGE, Morogoro: Rest in peace! Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Joachim Liyumba (68), aliyefariki Aprili 18 na kuzikwa wikiendi iliyopita kijijini kwao, Kwiro, Mahenge Wilaya ya Ulanga mkoani hapa huku mambo manne yakiwastaabisha waliojitokeza kwenye mazishi hayo. Mwili wapokelewa kwa ngoma ya baba yake Liyumba, ni ngoma aina ya Sangora. Ngoma yakesha Wombolezaji wakiwasili kanisani kwa ajili ya maombezi ya ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Liyumba. Wakiwa njiani kuelekea kanisani…. Mwili wa Liyumba wabadilishwa kutoka gari la kwanza na kuwekwa kwenye gari la wagonjwa kisha kuelekea katika Kanisa la Parokia ya Kwiro, Jimbo la Mahenge. Padri Filbert Mhasi akiendesha ibada Mazishi yake yahudhuriwa na watu wachache. Chanzo chabainika kwa nini...

JPM Ateua Makatibu Tawala wa Mikoa 26

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Aprili, 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara. Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, 2 wamebadilishiwa vituo vya kazi na 13 wamebakisha katika vituo vyao vya sasa. Makatibu Tawala wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo;     1. Arusha –    Richard Kwitega     2. Geita –      Selestine Muhochi Gesimba     3. Kagera –     Armatus C. Msole     4. Kilimanjaro –    Eng. Aisha Amour     5. Pwani –      Zuberi Mhina Samataba     6. Shinyanga –   Albert Gabriel Msovela     7. Singida – ...

BREAKING NEWS : CAG ATAJA MAJIPU SUGU KWA TAIFA

Image
========= UPDATES: ========= => Ulaji na uzembe vinatajwa kubeba sehemu kubwa ya ripoti hii. => Misamaha ya kodi 2014/15 ni asilimia 2 ya pato la taifa kinyume cha asilimia 1 => Halmashauri 40 hivi ndo zenye hati safi kati ya halmashauri zaidi ya 160 => Bidhaa a bilioni 9 za kupelekwa nje ziliuzwa hapa hapa nchini. Upigaji huo wa ukwepaji kodi. => Bidhaa za bilioni 89 za nje hakuna ushahidi kama zilienda Rwanda, Burundi na Uganda. => Rufaa za kodi nyingi mno zimedoda mahakamani na hivyo kuikosesha serikali kodi => Deni la Taifa hadi Juni 2015 lilifikia trilioni 33.5. Ndani ya mwaka mmoja lilikua kwa trilioni 7! => Malipo kwa deni kwa mwaka ni trilioni 4. => Deni na mishahara inamaliza mapato yote ya taifa. CAG anahoji, tutapata wapi pesa za maendeleo? => CAG Anataka maduka ya fedha za kigeni yadhibitiwe => Vyama vya siasa, kimoja tu kimewasilisha hesabu. Vyama 21 bado, Msajili afiatilie. Hajakitaja chama kilichowasilisha => Mishahara hewa ka...