WEMA SEPETU AIPASUA KATIKATI CLUB YA BONGO MOVIE BAADA YA RAY KUWAKATAZA WASANII WASIHUDHURIE MSIBA WA BABA YAKE
Wema Sepetu Klabu ya Bongo Movie ambayo inaundwa na baadhi ya wasanii wa filamu Swahiliwood imepasuka katikati kisa kikidaiwa kuwa ni lile tamko linalodaiwa kutolewa na mwenyekiti wa klabu hiyo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kuwa mwanachama yeyote wa kundi hilo asitie miguu kwenye msiba wa baba mzazi wa mwenzao, Wema Sepetu, marehemu Balozi Isaac Sepetu. Tukio hilo la katazo lilitokea wakati wa maombolezo ya kifo cha mzee Sepetu kilichotokea Oktoba 27, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ kwa ugonjwa wa kisukari ambapo msiba ulikuwa nyumbani kwake, Sinza Mori jijini Dar es Salaam. LAWAMA ZOTE KWA RAY Kufuatia madai hayo, baadhi ya wasanii kutoka klabu ya Bongo Muvi (majina tunayo) wamekuwa wakitoa lawama zao kwa Ray huku wengine wakidai wamejitoa kwenye kundi hilo kwa sababu halina umoja na limejaa unafiki. Maneno hayo yalianza kusambaa baada ya Wema kumaliza kumzika baba yake Oktoba 31, mwaka huu mjini Zanzibar. Wema Sepetu (katikati) baada ya kuwasil...