Mpenzi wa Cristiano Ronaldo ametumia Kiswahili leo
Lugha ya Kiswahili inaonekana kuzidi kukuwa na kuwavutia watu mbalimbali dunia kuitumia, leo April 1 2018 moja kati ya post za mitandao ya kijamii zilizochukua headlines ni post ya mwanamitindo Georgina RodrĆguez ambaye ni mpenzi wa staa wa soka wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Georgina RodrĆguez ni mwanamitindo na ndio mpenzi wa sasa wa Ronaldo na wamefanikiwa kupata mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Alana Martina , hivyo katika insta story yake amepost picha yake na Ronaldo na kuandika āHakuna Matataā Msemo wa hakuna matata ni msemo wa Kiswahil i ambao umeonekana kupendwa na umekuwa msemo maarufu sana kwa wageni wanaopenda kujua lugha ya Kiswahili, huo huwa ni msemo wao wa kwanza kujifunza lakini haijajulkana bado Georgina RodrĆguez ameujulia wapi msemo huo.