Posts

Showing posts from February 18, 2015

MZEE YUSUPH KUOA MKE WA TATU

Image
Mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusuph anatarajia kuoa tena mke wa tatu hivi karibuni huku wake zake wawili wakiwa kwenye bifu zito wakitupiana vijembe mtandaoni. Akipiga stori na Uheard na Soudy Brown alisema kuwa anatarajia kuoa mke huyo ambaye anaishi huko visiwani Pemba,na kwamba mipango ikiwa tayari kila kitu kitakuwa hadharani. Hivi karibuni wake zake wawili ambao ni Malkia Leila Rashid ambaye pia ni mwimbaji wa kundi hilo na mke wake mdogo aitwaye Chiku wamekuwa wakirushiana vijembe kwenye mtandao wa kijamii wa ‘Whatsap’ kwa kuandikiana ‘Status’ za vijembe. Habari zinasema kuwa wake hao wamekuwa kama chui na paka na mzee Yusuph hana mpango wa kuwapatanisha kwa kuwa hakuna hata mmoja aliyeonyesha chuki kwa mwenzake akiwa na nao. 

BREAKING NEWZ:RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27, PAUL MAKONDA NA FREDRICK MWAKALEBELA NDANI

Image
Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani. Mkuu mpya wa Wilaya ya Wanging’ombe, Fredrick Wilfred Mwakalebela. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12. Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42. Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; ...

ANGALIA WADADA JINSI WANAVYOFANYIWA HUKO CLUB

Image

Majambazi yafunga mtaa jijini Mwanza na kuua mtu mmoja

Image
Matukio ya ujambazi na mauaji ya kutumia silaha, yameanza kuibuka kwa kasi katika maeneo mbalimbali nchini.   Hali hiyo imekuwa ikihojiwa na wananchi na wapenda amani na zaidi ni kuhusu intelijensia ya polisi kushindwa kugundua mipango ya uhalifu.   Wachunguzi wa mambo wanasema kuwa kushamiri kwa matukio hayo kunaleta hofu katika jamii huku jamii yenyewe ikilaumiwa kwa kukaa kimya kwa watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na hutumia isivyo halali.   Hali hiyo imetokea mjini Magu, mkoani Mwanza kwa watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa na silaha za moto usiku wa kuamkia jana walifunga Mtaa wa Kisesa Kata ya Kisesa, Wilaya ya Magu mkoani Mwanza na kumuua mfanyabiashara Nestory Andrew umbali wa mita 50 kilipo Kituo cha Polisi.   Tukio hilo lilitokea saa 8:00 usiku, majambazi hayo yalifunga Barabara ya Mwanza-Musoma kwa muda na kusababisha taharuki kwa wakazi wa Kisesa huku milio ya bunduki ikitawala anga.   Wakizungumza ...

Labda ulikua huyajui haya kuhusu hizi picha za Wema Sepetu na Ommy Dimpoz

Image
Zile picha za mahaba zilizosambaa kwenye mitandao zikimuonyesha Staa wa Bongo Fleva,Ommy Dimpoz na Wema Sepetu wakiwa kitandani zimezidi kuzua utata baada ya Ommy kusema hakujua alipigwa saa ngapi kwani hakuwa na fahamu bali aulizwe Wema.Ommy amezungumza na Uheard na Soudy Brown alisema kuwa hana maelezo zaidi ya kuzungumza zaidi ya kusema kuwa hajui ni muda upi zilipigwa picha hizo.Wiki hii picha hizo zilisambaa mitandaoni na kuzua hizo zilisambaa mitandaoni na kuzua maswali kuwa Ommy Dimpoz ameamua kujiweka kwa Wema baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platinum,lakini Aunty Ezekiel ambaye rafiki wa Wema alisema kuwa rafiki yake huyo alikwenda nchini Afrika Kusini kufanya video mpya ya ngoma ya Ommy. Hata hivyo picha nyingine zilisambaa Wema akiwa na aliyekuwa mume wa Zari wakiponda raha nchini humo na kuzua sintofahamu.

Mchumi wa Wizara ya Ardhi Afikishwa Mahakamani akituhumiwa Kumshika Matiti Mwanamke bila Ridhaa Yake

Image
MCHUMI wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Brown Kajange (42) amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo kujibu mashitaka mawili, likiwamo la shambulio la aibu kwa kumshika matiti mwanamke bila ridhaa yake. Karani wa Mahakama hiyo, Blanka Shao alidai mahakamani hapo mbele ya Hakimu Matrona Luanda kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Februari 16, mwaka huu katika eneo la kuuzia samaki la Feri Kivukoni wilaya ya Ilala. Shao alidai siku ya tukio saa 6 mchana katika eneo hilo, mshtakiwa alimshika matiti Queensia Fusi bila ridhaa yake huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria. Alidai kuwa shtaka la pili, mshtakiwa alimpiga ngumi mlalamikaji katika jicho la kushoto na kusababisha maumivu makali katika sehemu hiyo. Mshtakiwa alikana mashtaka na Hakimu Luanda aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 3, mwaka huu itakapotajwa. Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka serikali ya...

CHADEMA YAWAPIGA "STOP" WANAOTAKA KUWANG'OA LEMA NA NASSARI

Image
Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe akiwa pamoja na Mbunge Joshua Nassari (kushoto) na Godbless Lema (kulia) katika moja ya mikutano ya chama hicho. Picha ya Maktaba  Chama cha Demokrasia na Maendeleo(chadema), mkoa wa Arusha “kimewapiga stop” wanachama wake, kutangaza nia ya kugombea ubunge katika majimbo matatu, yanayoshikiliwa na wabunge wa chama hicho,hadi hapo Bunge litakapovunjwa rasmi julai 2 mwaka huu. Majimbo hayo ni jimbo la Arusha mjini, mbunge wake, Godbless Lema, Jimbo la Arumeru Mashariki, mbunge Joshua Nassari na Jimbo la Karatu mbunge, Mchungaji Israel Natse ambapo tayari kuna    wanachama wa chama hicho, wameanza kutangaza nia   za kuwang’oa wabunge hao. Akizungumza na mwananchi leo, Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Calist Lazaro alisema, maagizo anayoyatoa ni kutekeleza utaratibu ambao umetolewa na Kamati Kuu ya chama hicho,kuhusiana na uchaguzi mkuu ujao. “Naomba hapa ieleweke kuwa hatuzuwii...

TEAM WEMA WAMKANA OMMY DIMPOZ, WEMA ANAYE MPENZI WAKE HANDSOME BOY

Image
Kubwa la Maadui Dougiemasta wa Instagram Ambaye kwa sasa ni Kiongozi wa Team Wema Sepetu amefunguka Kuhusu wale wanaotaka kujua kama wema ana mpenzi ama la kwa sasa baada ya kuachana na Mwanamuziki Diamond Platnumz...Haya ndio aliyoyasema: 'Kabari habari zenyu wananchi.kwa watu jana wameni uliza kwanini wema ajamuonesha mpenzi wake na wala ajaonesha wapi walikwenda kwenye valentine day banange kwani ukipiga picha halafu umepozi kama uko kwenye mahaba kwaiyo hapo inamaanisha kuwa mnapenda sana ? just picha aina maana yoyote. Valentine day sio lazima utoke out na mpenzi na vitu fulani una weza kukaa home na unayempenda basi maisha yanakwenda. Haya mapenzi ya mitandao yasiwasumbue akili zenu watu wanatumia pesa nyingi kuonesha wapizani wao kuwa wao wanapenda Nakumbukeni kuwa wema alisema mwaka huu anataka kujifunza yale makosa yako yote ,wema yupo bussy sana na mambo ya kikazi na biashara kuweni wavumilivu mtaona vitu vyake mwaka huu.Wema Sepetu anaye mupenzi wak...

Ndesamburo njiapanda

Image
Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo    Ashikwa kigugumizi kugombea tena ubunge, CCM yatamba kumweka mgombea anayekubalika Moshi Mjini. Moshi. Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo ana siku 72 za kuamua kugombea tena kiti hicho au la, ili kupisha wanachama wengine watangaze nia. Ndesamburo anaonekana yuko njiapanda kutoa uamuzi, huku taarifa zilizozagaa zinadai kwamba hagombei tena. Mbunge huyo ni miongoni mwa wabunge wakongwe wa upinzani, tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1991. Ndesamburo ambaye amekuwa mbunge kwa vipindi vitatu vya kuanzia mwaka 2000 hadi 2015, alipotafutwa jana kuzungumzia tetesi hizo alisema: “Wakati ukifika nitasema kama nagombea au sigombei.” Kutokana na kuzagaa kwa taarifa hizo, Chama cha Mapinduzi (CCM) kinadaiwa kusubiri kwa hamu tamko la Ndesamburo, ambaye amekisumbua chama hicho kwa miaka 15 mfululizo. Katibu wa Chadema, Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema alikiri...

Mama aliyeporwa mtoto albino afanyiwa upasuaji wa kichwa

Image
Ester Jonas (30) ambaye ni mama mzazi wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Yohana Bahati akiwa amelazwa kwenye chumba cha uangalizi maalumu katika Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC). Picha na Aidan Mhando Wabunge walia na Serikali kushindwa kulifanyia kazi tatizo la utekaji na mauaji yanayoendelea Geita/Dar. Mama wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ambaye alitekwa juzi na watu wasiofahamika mkoani Geita, amefanyiwa upasuaji wa kichwa na jopo la madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) mjini Mwanza. Mama huyo aliyefahamika kwa jina la Ester Jonas (30), alilazimika kufanyiwa upasuaji huo baada ya kushambuliwa kwa kukatwa mapanga na watu hao ambao walimteka mtoto wake juzi akiwa amembeba mgongoni nyumbani kwake. Mkuu wa Kitengo cha dharura cha Hospitali ya Bugando, Dk Darick David alisema mama huyo alifikishwa hapo jana akiwa na hali mbaya kutokana na kuvuja damu nyingi. “Namkumbuka mwanangu Yohana Bahati,” hayo ni maneno aliyoyasema mama mzazi wa mtoto huyo a...

Bunduki Waliyoporwa Polisi na 'Magaidi wa Tanga' Yapatikana ikiwa na Risasi 20......Ilikuwa Imefichwa ndani ya Mapango ya Amboni

Image
Polisi  mkoani Tanga imesema imefanikiwa kupata bunduki aina ya SMG, ikiwa na risasi 20 ndani ya mapango ya Majimoto katika eneo la Amboni, inayodaiwa ilikuwa ikitumiwa na wahalifu waliorushiana risasi na askari mwishoni mwa wiki.   Aidha, imesema inashikilia watu kadhaa akiwemo aliyesababisha kupatikana kwa bunduki hiyo. Baadhi ya watu wanaendelea kuhojiwa, kupata taarifa kwa lengo la kukamata waliopora silaha kwa askari na kurushiana risasi kwenye mapango hayo.   Kupatikana kwa silaha hiyo, kunafuatia msako maalumu uliodumu kwa siku nne sasa, uliolenga kusaka silaha na wahalifu wanaodaiwa kujificha ndani ya mapango ya mawe yaliyopo Amboni, nje kidogo ya mji wa Tanga.   Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja alitoa taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari mjini hapa.   Alisema mafanikio hayo, yametokana na subira ya wakazi wa Tanga na ushirikiano mkubwa wanaoendelea kuuonesha kwa Polisi inayos...