‘Vita’ ya Alikiba na Samatta Imefika Pabaya
NAHODHA wa Timu ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars na Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta ameingia kwenye vita ya ki-sport na msanii wa Bongo Fleva, Alikiba inayotarajiwa kufanyika Juni 9, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhamasisha uchangiaji wa vifaa na miundombinu katika mashule. Samatta amesema mechi hiyo itakuwa itamuhusisha yeye na marafiki zake dhidi ya Alikiba na marafiki zake pia. “Itakuwa mechi ya hisani kama zilizo nyingine ambazo zimekuwa zikifanywa na wachezaji wakubwa, hii ni kati ya Samatta 11 na Alikiba 11, nitachagua marafiki zangu na Kiba atachagua marafiki zake. Nataka nifanye moja lakini itakuwa na radha tofauti, kwani timu pinzani itakuwa ya Alikiba. “Ok, nimepewa jukumu la kuandaa jeshi la maangamizi mchezaji gani ungependa kumuona siku iyo awe wa sasa au wa zamani?” amesema Samatta. Alikiba amesema amefurahi urafiki wake na Samatta kuzalisha kitu hicho kizuri huku akiwaomba wapenzi n...