Posts

Showing posts from May 21, 2016

JE, UNA HERUFI M KATIKA KIGANJA CHAKO? HII NDIO MAANA YAKE

Image
Watu wengi wanasema, mistari katika viganja vya kila binadamu vimebeba mambo mengi na maana nyingi kuhusu tabia yako na hatima yako kwa ujumla. Pia inasemekana watu wenye herufi 'M' katika viganja vyao,ni watu wa aina muhimu sana.Inasemekana watu hawa wana sifa za ajabu.Wana ushirikiano mzuri na wafanyakazi katika aina yeyote ile ya biashara. Kama una mpenzi mwenye alama 'M' katika kiganja chake,basi yakupasa kujua yupo makini katika uhusiano wenu.Hakuna utani,hakuna uongo na hakuna udanganyifu. Watu wenye herufi 'M' katika viganja vyao, wana uwezo mkubwa wa kufanya mabadiliko katika maisha yao na daima utumia vizuri fursa wanazozipata katika maisha yao. Imekuwa ikijulikana kwa watu wa zamani, kwamba manabii wote walikuwa na alama hii katika mikono yao. Angalia mkoni wako na endapo ukijikuta una alama ya 'M' basi tambua kwamba wewe ni mtu maalamu

Kumbukumbu ya Kuzama kwa Meli ya MV Bukoba Mei 21, 1996

Image
Meli ya MV Bukoba ikwa Ziwa Victoria wakati ilipokuwa ikitoa huduma ya usafirishaji kabla ya kuzama. KIUKWELI tarehe kama ya leo miaka 20 iliyopita haitoweza kusahaulika kirahisi kwenye mioyo ya Watanzania na Ulimwenguni kote, kwani usiku wa kuamkia Mei 21, 1996, meli ya MV Victoria ikiwa na abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37 ilizama majini kwenye Ziwa Victoria mwambao wa Bwiru Jijini Mwanza ambapo ilikuwa takribani kilomita 30 kufika nchi kavu. Meli ya Mv Bukoba ikiwa inazama. Ripoti ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha hiyo ilieleza kuwa, kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma barabara ya Musoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana. Kila mwaka, ifikapo Mei 21, viongozi wa dini, wa serikali na wananchi huongozana kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu. Mnara wa Kumb...

WAZIRI MKUU AFAFANUA KUHUSU KUTENGULIWA KWA UTEUZI WA WAZIRI KITWANGA

Image
Mh. Charles Kitwanga aliekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.  “Zipo sheria za utumishi ambazo mtumishi hatakiwi kunywa pombe na wala hapaswi kulewa akiwa kazini… mtumishi anapaswa kuwa na akili timamu inayokuwezesha kufanya kazi za Serikali,” alisema.  Ametoa ufafanuzi leo usiku (Ijumaa, Mei 20, 2016) wakati akijibu swali la mwandishi wa TBC1aliyetaka kujua kama taarifa zilizoenea kuhusu kutenguliwa kwa Waziri huyo ni za kweli.  “Ni kweli Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016 baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake leo asubuhi,” alisema Waziri Mku...

Tanzia: Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar, Wilson Kabwe Afariki Dunia

Image
  Marehemu Wilson Kabwe. ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amefariki usiku wa kuamkia leo nchini India alikokuwa ameenda kutibiwa. Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Rais John Pombe Magufuli, Aprili 19 alimsimamisha kazi Bw. Wilson Kabwe kutokana na ufisadi katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya jiji na  kuisababishia  serikali  hasara  ya  pesa zaidi ya bilioni 3. Rais Magufuli alichukukua uamuzi huo siku ya uzinduzi wa daraja la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda alitoa hotuba fupi ya maswala kadhaa ya Mkoa wa Dar es Salaam  ikiwemo  ripoti ya tume aliyounda  kuchunguza utekelezwaji wa mikataba hiyo. Kabla ya kuhamishiwa jijini Dar es Salaam, Kabwe ali...

A-Z Shoo ya Jide Mlimani City

Image
Malkia wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee usiku huu amefunika vilivyo katika shoo yake ya Nasimama Tena iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City. Staa huyo akiwa na vijana wake wamepiga shoo kali ya Live iliyochukua saa tatu na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki walioshindwa kujizuia kukaa kwenye viti vyao na kunyanyuka mara kwa mara kwenda stejini kucheza nyimbo mbalimbali za malkia huyo. Shoo hiyo imehudhuriwa na mastaa kibao wa Bongo Fleva na Bongo Movies wakiwemo Alikiba, Idrisa Sultan, Wema Sepetu, Elizabeth Michael na wengineo kibao. Usikose kuangalia Global TV Online kuona video za matukio yote yaliyojiri. Picha: Clarence Mulisa, Gabriel Ng’osha na Rishard Bukos / GPL

MATUKIO YA BUNGENI LEO.

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akibadilishana mawazo na na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwa(kulia) jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge.   Afisa Habari wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Patson Sobha(aliyenyosha mkono) akitoa maelezo kwa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma walitembelea Bunge kama sehemu ya mafunzo jana mjini Dodoma.  Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu(kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Simanjirio Mhe. James Ole Milya(wa pili kushoto), Mbunge wa Tarime Vijijini Mhe.John Heche(wa pili kulia) na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwa(kulia) jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge.  Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe Venance Mwamoto(kushoto) jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bu...