HIKI NDO KIASI CHA PESA ANACHO INGIZA RAISI OBAMA KWA MWAKA
BAADA ya kuchaguliwa katika awamu ya pili ya utawala wa Marekani, Rais Barack Obama, ameendelea kupata mshahara wa dola 400,000 kwa mwaka. Wakati alipopata utawala, Rais huyo mwenye nguvu duniani ameendelea kuwa Kamanda wa Jeshi la Marekani, Rais mwenye nguvu duniani na ameendeleza utawala wa Air Force One. Obama alipoingia Ikulu kwa mara ya kwanza, kipato chake kilikuwa dola 1.3 milioni. Miaka minne baada ya kukaa Ikulu kipato chake kimeongezeka kwa asilimia 800 sasa anapata dola 11.8 milioni. Kipato kimeongezeka vipi? Awali Obama alikuwa na kipato kidogo, alikuwa akilipwa dola 60,000 kwa mwaka alipokuwa Seneta wa Illinois na baadaye akawa analipwa dola 175,000 kwa mwaka. Jambo la kufurahisha ni kuwa kabla Obama hajawa Rais, hakuwa na mshahara mkubwa, hata mke wake, Michelle, alimzidi kwa kipato. Michelle alikuwa akiingiza kiasi cha dola 320,000 kwa mwaka, wakati huo alikuwa Makamu wa Rais wa Kitengo cha U...