Breaking News: Sugu, Masonga Wahukumiwa Jela kwa Kumkashifu JPM
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga, wamehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli. Mahakama imetoa uamuzi huo leo Jumatatu, Feb. 26, 2018 na hakimu wa mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mhakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, Maiko Mteite, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka. Pia mahakama hiyo imemhukumu kifungo cha miezi mitano Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga, kwa kosa hilo. Washtakiwa hao wanatajwa kutenda kosa hilo Desemba 30, 2017 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya wakati wakiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara.