Mlezi wa Simba, Rahma Al Kharoosi 'Malkia wa Nyuki'. MLEZI wa Simba, Rahma Al Kharoosi, ametua jijini Dar es Salaam akiwa kwenye ndege kubwa yenye uwezo wa kubeba watu 150, lakini yeye akiwa ndiye abiria pekee ndani ya ndege hiyo. Rahma, maarufu kama Malkia wa Nyuki, ametua na ndege hiyo aina ya Airbus 320 inayomilikiwa na Serikali ya Oman na anaitumia yeye kupitia cheo chake cha Balozi wa Heshima wa Oman nchini Morocco. Ndege hiyo ilikuwa imebeba watu 17, kati ya hao 16 ni wafanyakazi ndani ya ndege ambao ni daktari mmoja, walinzi wanne, waliobaki ni marubani na wahudumu. Akizungumza dakika chache kabla ya kuondoka nchini jana, saa 10 alfajiri, Malkia wa Nyuki alisema alishuka nchini kwa ajili ya mapumziko ya siku moja, pia kuzungumza na baadhi ya viongozi wa Simba. āNimepita tu, tumepumzika kidogo hapa na baada ya hapo ninakwenda Comoro kwa ajili ya kuzungumza na kumchukua R...