Posts

Showing posts from March 24, 2016

Waholanzi Wawili Wakamatwa KIA na Tumbili 61

Image
Waziri wa Maliasili na Utalii Pro. Jumanne Maghembe. WAZIRI wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe leo amemsimamisha kazi Mkurugenzi Msimamizi wa Wanyamapori, Charles Mulokozi baada ya kutoa vibali vya kusafirisha Tumbili kwenda Albania. Sakata hilo limetokea baada ya Jeshi la Polisi kuwakamata raia wawili wa Uholanzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakiwa na tumbili 61 hai wakijaribu kuwasafirisha kwenda nchini Albania.

TUME YA UCHAGUZI YAKAMILISHA IDADI YA WABUNGE WA VITI MAALUMU WA TATU.

Image
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva akizungumza na waandishi wa habari na kutangaza Majina ya wabunge wa wa viti maalumu katika ukumbi wa tume ya uchaguzi jijini Dar es Salaam, kuhusiana na tume hiyo kukamilisha idadi ya wabunge watatu wa viti maalumu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wawili na wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema (Chadema) mmoja. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Givenes Aswile akiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo. Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva akitangaza majina ya wabunge wa viti maalumu watatu kuwa ni   Ritha Kabati (CCM), Oliver Semunguruka (CCM) pamoja na Lucy Owenya (Chadema). kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Emmanuel Kavishe. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva jijini Dar es Salaam leo wakat...

DK. SHEIN ALA KIAPO CHA URAIS WA ZANZIBAR

Image
Rais Mteule wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiapishwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo na Jaji Mkuu wa Zanzibar  Mhe,Omar Othman Makungu katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]

Lucy Komba azichapa Ulaya kisa, wivu

Image
Lucy Komba Imelda Mtema Msanii wa kitambo kunako filamu za Kibongo, Lucy Komba anayeishi Finland kwa sasa, amezichapa ‘live’ na rafiki yake kipenzi, Edina John huku kisa kikitajwa ni wivu wa mapenzi. Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na mashosti hao, kilimwaga ubuyu kuwa mapema mwezi huu, Lucy alimualika rafiki yake huyo nyumbani kwake kwa ajili ya kubadilishana mawazo kuhusu mambo ya filamu, nk. “Baada ya Edina kwenda kule walikuwa wakikaa nyumba moja na ikatokea mazoea makubwa kati ya mume wa Lucy na Edina kitu ambacho kilimpa wasiwasi Lucy. “Siku ya tukio Lucy alikuwa jikoni akipika huku Edina akipiga stori na mumewe sebuleni, alipopiga chabo alimuona shosti wake akiongea kwa kumrembulia macho mumewe tena wakiwa karibu akamfuata na kumrushia maneno machafu na kushikana ndipo mumewe akawaamulia,” kilisema chanzo. Baada ya Showbiz Xtra kunyaka ubuyu huo, lilimtafuta Lucy kwa njia ya WhatsApp ambapo alifunguka kwa kifupi; “ Jamani hayo mambo yameshapita kwanza haya...

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 24.03.2016

Image
                       

MAGAZETI YA MICHEZO LEO TAREHE 24/03/2016

Image

MAGAZETI YA UDAKU TRH 24.03.2016

Image

TRL KUSAFIRISHA SARUJI YA TANGA KWA NJIA YA RELI

Image
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigela akitoa taarifa ya hali ya miundombinu katika mkoa wa Tanga kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ofisini kwake. Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa pili kulia) akimwonesha moja ya nyaraka Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (wa pili kushoto) kabla ya kusaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa tatu kulia) pembeni ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tang...

WAZIRI LUKUVU AWATIA KITANZI NHC

Image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameiagiza bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa Nyumba (NHC) kuacha kuanzisha miradi mipya ya ujenzi hadi kukamilishwa kwa miradi iliyokwishaanza. Akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo Dar es Salaam jana, Lukuvi alisema hakuna haja ya kuanzisha miradi mipya wakati iliyopo haijakamilika. “Nadhani miradi iliyopo mnaijua na tarehe za kukamilika ujenzi wake wote tunafahamu, hivyo nitoe agizo kuanzia leo hakuna kuanza kwa mradi mpya wowote mpaka imalizwe iliyokwishaanza,” alisema. Lukuvi pia aliiagiza bodi hiyo kutopandisha kodi za nyumba zake bila ridhaa yake huku akisisitiza gharama zipangwe kwa kuzingatia uwezo wa wananchi. “Hamuwezi kusema nyumba ya gharama nafuu wakati ina vyumba viwili na inauzwa kwa Sh52 milioni, hainiingii akilini na wala Mtanzania wa kawaida hawezi kuona unafuu wowote hapo,” alisema Lukuvi.

RC KIJUU: WATUMISHI HEWA ANZENI KUJIONDOA KABLA SIJAWAKAMUA MAJIPU

Image
Mkuu  mpya  wa  Mkoa  wa  Kagera,Meja  Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amewaagiza  watumishi  wasio  na  sifa za  kuajiriwa kujiondoa  kabla  ya March  31  mwaka  huu. Kijuu  alitoa  kauli  hiyo  jana  wakati  wa  Makabidhiano  ya  ofisi baina  yake  na  mkuu  wa  mkoa  wa  zamani,John Mongella ambapo alisema  kwamba  Tanzania  inawatumishi  hewa  zaidi  ya 2000, hivyo ana imani  hata  Kagera  wapo. "Hao watumishi  hewa  endapo  watang'ang'ania kubaki katika vitengo  walivyopo  nitawashughulikia wahusika  wakuu  wa  vitengo  hivyo,"   alisema Aidha, aliagiza wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kusimamia uundwaji wa mabaraza  ya  usuluhishi kuanzia ngazi za kata hadi  mkoa  ili  kusimamia...

MAKABIDHIANO YA UONGOZI WA MKOA WA DODOMA

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akitoa salamu zake wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa wa Dodoma baina yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe Mhe. Chiku Gallawa (hayupo pichani) Machi 22,2016.   Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akitoa salamu zake wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa wa Dodoma baina yake na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (hayupo pichani) Machi 22,2016.   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa huo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Chiku Gallawa (wa tatu kushoto) Machi 22,2016   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (wa kwanza kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya...