WASTARA, CLOUD WAZURU MAKABURI YA WASANII WENZAO
Cloud, Mtitu, Wastara, Steve Nyerere, Barafu na Chiki katika kaburi la Adam Kuambiana. Wastara akilia kwa uchungu. Wastara na timu yake wakiweka mashada katika kaburi la Kuambiana. Kaburi la marehemu Adam Kuambiana. Wasanii katika kaburi la Steven Kanumba. Wasanii pia walitembelea kaburi la msanii mwenzao John Maganga. Mwisho kabisa wasanii walitembelea kaburi la Zuhura Maftah Malisa. WASANII wa Bongo Movie Unity ambao hawakuwepo katika msiba wa Adam Kuambiana wakiwa nchini Uingereza, Issa Mussa ‘Cloud’ na Wastara Juma leo wamezuru kaburi Kuambiana pamoja na makaburi ya wasanii wengine ambao tayari walishatangulia mbele ya haki akiwemo John Maganga, Steven Kanumba na Zuhura Maftah Malisa. Wakizungumza na waandishi wetu, wasanii hao wamesema kuwa ni jambo la kumshukuru Mungu lakini watazidi kuwaombea wale wote waliotangulia kwa kuwa wote wako katika njia moja.