Posts

Showing posts from October 8, 2017

Kichwa cha mwandishi aliyetoweka chapatikana baharini Sweden

Image
                 Kichwa cha mwandishi wa Sweden Kim Wall kimepatikana , miezi miwili baada ya kupotea katika ziara na raia mmoja wa Denmark. Waogeleaji walipata mifuko iliokuwa na kichwa chake, miguu na nguo katika eneo la Koge Bay kusini mwa mji wa Copennhagen kulingana na inspekta mkuu wa polisi wa eneo hilo Jens Moller Jensen. Vilipatikana karibu na pale mwili wa Wall ulipokuwa siku chache tu baada ya kupanda katika manuwari tarehe 10 Agosti. Bwana Marsden mwenye umri wa miaka 46 amekana kumuua bi Moller Jensen akisema mabegi hayo yaliopatikana yalikuwa yamechanganywa na kupimwa uzani na vipande vya vyuma. ”Jana alfajiri tulipata begi ambalo lilikuwa na nguo za Kim, suruali ya ndani na viatu.katika begi hilo hilo kulikuwa na kisu na kulikuwa na mabomba ya magari” . Matokeo ya uchunguzi yamebaini kwamba kichwa hicho ni cha bi Wall na kwamba hakina ishara za kwamba fuvu lake la kichwa liliumizwa ama hata kupigwa.   Matokeo hayo yanaenda kinyume na taarifa za

Sirro Asema Hataki Malumbano Kuhusu Kushambuliwa Lissu

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro. Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amesema hataki malumbano na hana majibu kuhusu shinikizo linalotolewa na Chadema na familia ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuruhusu vyombo vya nje kufanya uchunguzi wa tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi kwa mbunge huyo. IGP Sirro amesema hayo leo Jumapili jijini hapa, akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alipojibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua kauli yake baada ya familia ya Lissu na viongozi wa Chadema kutamka kuwa hawana imani na Jeshi la Polisi kuhusu uchunguzi huo. Lissu ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) alijeruhiwa kwa risasi Septemba 7 mjini Dodoma na sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya. IGP Sirro amesema yeye na jeshi lake wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria kwa kuwatumikia Watanzania wote kuhakikisha wanakuwa sala

ZARI THE BOSS LADY AKATA MZIZI WA FITNA,AIBUKA NA KUJIBU YOTE LIVE

Image
                 Mpenzi wa Diamond Platnumz, Zarina Hassan maarufu kama Zari The Boss Lady amefunguka na kudai kuwa yeye na mpenzi wake huyo hawajaachana. Akiongea katika U-Heard ya Clouds FM, Zari amedai kuwa hawajaachana kama inavyodaiwa na watu hii ni kutokana na kuwa hakumu-wish happy birtday katika mitandao ya kijamii kama ilivyozoeleka. Hakuna lolote baya linaloendelea kati yake na Diamond, na wanaheshima mikataba aliyonayo na kampuni pia hakuna chochote kibaya kinachoendele,” ameema mrembo huyo. Pia akaongeza kuwa “Nilimu-wish siku yake ya kuzaliwa sema nilitumia njia ya kawaida,na tunajaribu kuhamisha maisha yetu katika mitandao kuwa ya kawaida. Vile vile mrembo huyo alisisitiza kuwa stori zinazoenezwa kuwa Nillan sio mtoto wa Diamond sio za kweli na kuhusu DNA pia sio kweli.

BREAKING NEWS : AJALI MBAYA YA GARI NA TRENI TANGA LEO

Image
Gari iliyokuwa kuwa imepakiza watoto imezima kwenye kivuko cha Kwaminchi na kugongwa na treni. Watoto wawili waliokuwa wamekaa mbele walinusurika kifo baada ya dereva kuwaambia waruke, ila waliumia na kukimbizwa Hospitali.

IGP SIRRO AWAJENGEA UWEZO ASKARI WA MBEYA

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akisalimiana na waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya, aliokutananao Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo leo, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Katibu Tawala mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja na kamanda wa Polisi mkoani humo (DCP) Mohamed Mpinga, wakiwa katika picha na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa baada ya kikao kazi cha kubadilishana uzoefu katika kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akikagua gwaride maalumu aliloandaliwa kwa ajili yake alipowasili mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na askari wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wa kutumia silaha za moto cha mk