Posts

Showing posts from April 29, 2016

BREAKING NEWZZZZ…JAMBAZI SUGU LAKAMATWA POSTA ,WAWILI WAKIMBIA..NOAH YAKAMATWA

Image
MTU MMOJA ANAYE SAKIKIKA KUWA JAMBAZI AMEKAMATWA JIJINI DAR MAENEO YA POSTA BAADA YA KUTAKA KUMTAPELI MAMA MMOJA ANAYE FANYA KAZI YA TIGO PESA …MASHAHIDI WALIO KUWEPO ENEO HILO WANASEMA HUYO KIJANA ALIFIKA KWA DADA HUYO KWA LENGO LA KUTAKA KUWEPA PESA KIASI CHA TSH.ELFU TANO ..WAKATI YULE DADA ALIKUWA ANAHESABU PESA ZAKE KWANZA NDIPO HUYO JAMBAZI AKAKWAPUA NA KUKIMBILIA NDANI YA GARI AINA YA NOAH..NA KUMRUSHIA MTU ALIYEKUWA NYUMA YA HILO GARI….WAKATI HUO MCHEZO UKIENDELEA NDIPO DEREVA AKAWA ANAJIANDAA KUWASHA GARI NA KUONDOKA NDIPO RAIA WAKAMDAKA DEREVA NA KUMTOA KWENYE GARI …LAKINI DEREVA NA YULE ALIYEPOKEA PESA AKACHOROPOKA ..ILA YULE ALIYEIBA AKANASWA NDO HUYO KWENYE PICHA

Edward Lowassa na Mh.Sumaye kutua kwa kishindo Dodoma leo, bunge lahaha

Image
Aliyekuwa mgombea wa urais wa UKAWA Mh. Edward Lowasa na mwanamkakati wake waziri mkuu mstaafu Mh. Sumaye, wanatarajiwa kutua Dodoma leo kwa shughuli maalum ya kisiasa Taarifa za awali zinasema watakutana na wabunge wa UKAWA kimkakati. Tetesi zinasema kuwa Lowasa ataweka wazi “facts” kwa umma, kina nani wanahusika na kwa nini Bunge halionyeshwi live na kuwataka wananchi kuchukua hatua. Ikumbukwe pia kuwa juzi kati CAG alitoa repoti yake na kuonyesha madudu ya serikali chini ya CCM huku akizivua nguo tawala ya awamu ya nne na awamu ya tano kwa kushindwa kusimamia matumizi ya rasilimali.

Naibu Spika Achafua Hali ya Hewa Bungeni Baada ya Kumwita Mbunge BWEGE.

Image
Naibu Spika Tulia Ackson, ambaye katika vikao vya Bunge anatakiwa kusimamia mijadala kwenye chombo hicho cha kutunga sheria, jana alizua kizaazaa baada ya kumuelezea mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Selemani Said Bungara kuwa ni bwege, akimtaka aache kuonyesha hali hiyo. Kwa mujibu wa toleo la pili la Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Oxford) la mwaka 2004, neno bwege linamaanisha “mtu mjinga, mpumbavu, bozi, fala gulagula”. Kitendo cha kutumia neno bwege kumuelezea mbunge huyo kilisababisha wapinzani wacharuke, na kuibua bungeni kesi ya mtu aliyefunguliwa mashtaka mkoani Arusha kwa kosa la kumuelezea Rais John Magufuli kuwa ni bwege. Bila ya kuruhusiwa, mmoja alifungua kipaza sauti na kusema:  “Hatimaye msamiati wa bwege watua bungeni sasa kutumika rasmi. Futa lugha ya kuudhi; bwege bwege.” Hata hivyo, wabunge hao wa upinzani hawakushinikiza Dk Tulia kufuta kauliz yake, lakini baadaye wakiwa nje ya ukumbi waliponda kitendo hicho cha kiongozi huyo wa Bunge ambaye aligomb...

ZITTO KABWE : WAHUSIKA WA SAKATA LA TEGETA ESCROW WABURUZWA MAHAKAMANI.

Image
MBUNGE wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo) ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuwafikisha mahakamani wahusika wa sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow ili sheria ichukue mkondo wake. Zitto aliyasema hayo bungeni mjini hapa jana wakati akichangia kwenye hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, iliyowasilishwa na Waziri Angela Kairuki pamoja na ile ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), iliyowasilishwa na Waziri wake, George Simbachawene. Alisema mwaka 2014, Takukuru waliijulisha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwamba ilikuwa inachunguza na kumaliza uchunguzi kuhusu miamala ya kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenda Benki ya Stanbic Tanzania. Alisema katika taarifa zote ambazo Takukuru inatoa kuhusu kesi za ufisadi, hakuna mahali inapozungumzia maendeleo ya suala hilo. “Hata siku moja hakuna mahala Takukuru wanasema kuhusu uchunguzi huu na lini wahus...