MAAMUZI YA RAIS KUUPANDISHA HADHI MJI WA DODOMA KUWA JIJI NI SAHIHI-MAJALIWA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni Jijini Dodoma Mei 3, 2018. WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema maamuzi ya Rais Dkt John Magufuli ya kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji ni sahihi na ameyafanya kwa wakati muafaka na hakuna sheria iliyokiukwa. Aprili 26, 2018 Rais Dkt Magufuli aliupandisha hadhi mji wa Dodoma kutoka Halmashauri ya Manispaa na kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na kumteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 3, 2018) wakati akijibu swali la Bibi Felista Bura (Viti Maalumu) katika kipindi cha Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Bungeni Jijini Dodoma. Bibi Felista alitaka kupata kauli ya Serikali juu ya baadhi ya watu wanaobeza maamuzi ya Rais Dkt. Magufuli ya kuupandisha hadhi mji wa Dodoma. Amesema kuwa Rais Dkt Magufuli hakukiuka sheria kwa sababu a...