ANGALIA PICHA ZA AJALI MBAYA KATIKA MSAFARA WA RAIS KIKWETE HUKO GEITA NA ILIYOJERUHI WATU 5
Msafara wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk JakayaKikwete mkoani Geita, leo umeingia dosari baada ya gari moja lilokuwa kwenye msafara huo kupinduka na kujeruhi watu watno. Gari la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja wa MSD Kanda pamoja na waandishi wa habari.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Geita Lenard Paul ajali hiyo imetokea leo saa 3 na dakika 45 asubuhi katika eneo la Nyankumbu kilomita 3 kutoka makao makuu ya mkoa wa geita. Kamanda Paulo amesema gari hilo namba DFP.9730 aina ya Toyota Landcruzer lililokuwa likiendeshwa Yungi Mkwati, mali ya Bohari kuu ya Madawa (MSD), lilipinduka baada ya kuteleza kwenye lami iliyomwagwa barabarani hii leo. Amewataja Waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni mwandishi Peter Makunga wa Radio Kahama Fm na Radio Free Afrika, Peter Fabian wa Gazeti la Rai, Frederick Katulanda Moderator wa Tovuti ya mabadiliko.com, meneja wa MSD kanda ya Ziwa Byekwaso Tabura pamoja na dreva wa gari hilo Yu...