Posts

Showing posts from September 6, 2013

Msikiti wa Answar Sunna ulipo mjini DODOMA wateketea kwa moto mchana huu.

Image
Msikiti mkubwa wa  Answar Sunna  uliopo  barabara ya saba mjini Dodoma  umewaka  moto  mchana  huu  ikiwa  ni  muda  mfupi  baada  ya  swala  ya  mchana  kumalizika.... Akiongea  kwa  njia  ya  simu  na  Mpekuzi wetu, mmoja  wa  mashuhuda  walioshuhudia  tukio  hilo  amedai  kuwa  chanzo  cha  moto  huo  ni  moto wa  JIKO  la  wakazi  wa    ghorofa ya  juu  ya  jengo  la  msikiti  huo... Hata  hivyo, shuhuda  mwingine  aliyeongea  na  mtandao  huu  amedai    kuwa  chanzo  cha  moto  huo  ni  hitilafu  ya  umeme  iliyoanzia  ghorofa  ya  juu  ya  jengo  hilo.   Kwa  mujibu  wa  mashuhu...

Picha tano za yule daktari FEKI aliyenaswa katika hospitali ya KCMC

Image
      Daktari feki aliyenaswa katika hosptali ya KCMC aliyetambulika kwa jina la Alex Massawe akiwa amefungwa pingu mikononi mwake katika eneo la hosptali hiyo. Daktari Feki akisindikizwa na baadhi ya wafanyakazi wa hosptali ya KCMC kutoka katika moja ya wodi ambayo alikuwa 'akihudumia'. Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo (kushoto) akimwonesha Daktari Feki, Alex Massawe. Daktari Feki akiwa katika gari la polisi tayari kupelekwa kituoni. Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi, jana ulimnasa 'Daktari Feki' aitwaye Alex Sumni Massawe (33). Massawe alikamatwa saa 5:00 asubuhi ndani ya hospitali hiyo na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa makachero wa Jeshi la Polisi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia. Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amepanga kumfanyia upasuaji wa ngozi, Makasi Tipesa ambaye anasumbuliwa na ugonjwa huo baada ya kukutana na mama yake na kumuahidi kumpatia huduma kwa malipo ya Sh. 200,000. Habari zin...

Daz Baba achanganyikiwa na kuwa KICHAA... wadau wasema ni Bangi na Madawa ya kulevya

Image
Habari kutoka kwa chanzo cha uhakika zinadai kuwa msanii wa zamani wa kundi Daz Nundaz na hitmaker wa ‘Figure Namba 8′ Daz Baba amechanganyikiwa kutokana na hivi karibuni kuonekana akifanya vitendo ambavyo havilingani na mtu mwenye akili timamu. Chanzo hicho kimesema Daz alionekana maeneo ya Morogoro akiwa katika hali iliyowatia mashaka ndugu, mashabiki wa muziki pamoja na wasanii wenzake. Rafiki wa karibu na Daz Baba amemwambia  mwandishi wetu  jana akiwa mkoani Morogoro kuwa hali ya msanii huyo ni mbaya na ana dalili zote za mtu ambaye  ni  Kichaa na amekuwa mtu wakuzunguka barabarani huku akifanya matukio ya ajabu. “Hivi juzi juzi Daz alienda nyumbani kwa Afande usiku, akapiga kelele sana, Afande akaamka na kumkuta Daz akiwa mchafu na akiongea maneno ambayo hayaeleweki, baadaye alitaka kumfanyia tendo baya kwa mfanyakazi wa kike wa Afande lakini hakufanikiwa, ila watu wakajua kweli Daz hayuko sawa,” alisema. Baada ya taarifa hiy...

Ripoti maalumu ya gazeti la MWANANCHI kuhusu vurugu zilizotokea jana bungeni

Image
  Jana, Bingwa wa Dunia wa uzani wa kati (super middle), unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF), Francis Cheka alitembelea Bunge baada ya kutwaa taji hilo karibuni na jana hiyohiyo, Bunge hilo lilishuhudia ngumi kavukavu katika vurugu kubwa pengine kuliko zote zilizowahi kutokea katika ukumbi wake. Katika masumbwi hayo yasiyo rasmi, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anadaiwa kumpiga kichwa Askari wa Bunge na kumchania sare na kung’oa kipaza sauti. Mbilinyi jana alisema alikuwa anatafutwa na polisi huku akisema hilo limemshangaza akidai kwamba yeye ndiye aliyeshambuliwa na askari huyo. Vurugu hizo zilitokea baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuamuru kutolewa nje kwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe. Katika vurugu hizo Mbilinyi alibebwa juujuu na polisi hadi nje ya ukumbi...

Polisi na Mawaziri wadaiwa kujihusisha na biashara haramu ya NGONO

Image
BAADHI ya mawaziri na polisi wametajwa kuwa ni wateja wakubwa wa wanawake wanaouza miili yao, maarufu kwa jina la Changudoa. Hayo yameelezwa jana na Jukwaa la Wanaharakati Wanawake Vijana (YFF), walipokuwa wakiwasilisha ujumbe wao kwa njia ya sanaa ya ngonjera, katika tamasha la 11 la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) linaloendelea eneo la Mabibo jijini Dar es Salam. Wanaharakati hao wanawake vijana, walisema tatizo liko kwenye jamii ambayo inawahukumu changudoa bila kujiuliza kuwa wateja wao ni kina nani. ‘’… jamani hebu tuulizane, kwani changudoa mteja wake nani? Kwa taarifa yako, mawaziri, wabunge na mapolisi wamo; na hii ni changamoto kwa jamii,’’ walisema wanaharakati hao.   Akizungumza na Tanzania Daima baada ya kutoka jukwaani, kiongozi wa wanaharakati hao, Aisha Kijavala, alisema wameamua kutoa ujumbe huo kwa washiriki wa tamasha hilo ili jamii ijue wateja wa changudoa hao. Alisema wateja hao wakiacha kununua ngono, pia wanawake wanaouza m...