Posts

Showing posts from April 30, 2018

Breaking News: Mahakama Yaamuru Hans Pope na Lauwo Wakamatwe

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo April 30, 2018 imetoa amri kwamba Mwenyekiti wa Usajili wa Klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani ili kuunganishwa katika kesi inayomkabili Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’. Amri hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao. Wakili Swai amedai amewatafuta washtakiwa hao tangu Machi mwaka huu bila mafanikio hivyo akaomba hati ya kuwakamata washtakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani. Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, nyaraka na kutakatisha fedha kiasi cha Dola za Marekani 300,000.

Chadema Wakanusha Lissu Kuerejea Nchini

Image
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimekanusha taarifa zinazoendelea mitandaoni kuhusu uwezekano wa kurejea nchini kwa Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu kutokea Ubelgiji alipokuwa akipatiwa matibabu tangu mapema Januari mwaka huu. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA, Tumaini Makene amesema; Kupitia mitandaoni mapema leo kumekuwa na taarifa za kwamba Lissu anatarajiwa kutua nchini wakati wowote kuanzia juzi na kwamba amemaliza matibabu yake kitu ambacho si cha kweli na kimezua taharuki. Makene amesema, Lissu hajazungumza na mwandishi wa habari yeyote kuhusu kurejea kwake hapa chini kwa sababu  hajapona na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine mwishoni wiki hii au wiki ijayo. Chadema kimetoa wito kwa na wanachama na Watanzania wote wenye mapenzi mema kutokana na kuguswa na uzito wa masahibu yaliyompata Lissu wameendelea kuguswa na kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya matibabu na hali ya afya yake kupuuza taarifa hizo. Lissu yupo nchini Ubelgi

Makonda Ampokea Ahmed Aliyepooza Akitokea China

Image
Ahmed alikwenda nchini China miezi miwili iliyopita ambapo hali yake inaendelea vizuri  baada ya kupatiwa matibabu. Kijana huyo alipata tatizo hilo la kupooza baada ya kuumia wakati akifanya mazoezi ya kuogelea. Ahmed Albaiti akiwasili uwanja wa ndege Dar es Salaam akitoka katika matibabu nchini China leo. Picha na Denis Mtima | GPL