Posts

Showing posts from June 12, 2017

ACACIA Wapinga Ripoti ya Kamati ya Pili ya Rais JPM Kuhusu Mchanga wa Madini

Image
12 Juni 2017 Mwitikio wa Acacia kwenye matokeo ya kamati ya pili ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Acacia imeona matokeo ya kushtua ya kamati ya pili ya Rais iliyowasilishwa kwa Rais wa Tanzania Mh. Dk John P. Magufuli leo asubuhi ambayo imeangalia nyanja za historia za kiuchumi na kisheria ya mauzo ya nje ya makanikia ya madini. Kamati ya Pili imetoa matokeo yake kwa kutumia matokeo ya Kamati ya Rais ya Kwanza, iliyotangazwa tarehe 24 Mei 2017, ambayo Acacia imeikanusha vikali. Kamati hiyo ilipata matokeo yake kwa kutumia sampuli ya kontena 44. Kwa mujibu wa data za zaidi ya miaka 20 tulizonazo ni vigumu kuoanisha matokeo yetu na yaliyokutwa na kamati, na kamati imetoa thamani ya juu kwa zaidi ya mara 10 kuliko thamani halisi ya makanikia Kamati ya Pili inadai kuwa Acacia imetangaza kiasi cha chini cha mapato kuliko inavyopata na kulipa kodi kidogo kuliko inavyostahili kwa miaka mingi na kuficha mabilioni ya dola ya Marekani. Na hivyo imefanya mapen...

Spika Ndugai apigilia msumari Ripoti ya madini

Image
"Hakuna kitu kibaya kuwa katikati ya dhiki ambayo hukuistahili"-amesema Spika Ndugai baada ya kukabidhiwa ripoti ya pili ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais Magufuli kuchunguza sakata la mchanga wa Madini Leo Ikulu Jijini Dar es salaam "Haya ni mambo ya ajabu, ni mikataba ya kijinga na ya hovyo, Mimi na wabunge wenzangu wote kuhakikisha sheria zote zitakazoletwa tutazitendea haki"- Alisema Spika Ndugai Hatua hiyo imefuata baada ya Mapendekezo ya kamati ya hiyo iliyotaka sheria za nishati Madini zifanyiwe marekebisho ya haraka, ambapo Rais Magufuli ametaka bunge lifanye haraka iwezekanavyo.

Kilichouzwa nje ni Madini, Sio mchanga

Image
  "Biashara ya uuzwaji wa Makinikia haikufanyika kwa ushindani na si kweli kwamba wanauza Makinikia, kinachouzwa ni madini." amesema Mwenyekiti wa Kamati ya kuchunguza mchanga wa madini, Profesa Nehemiah Osoro Prof. Osoro ameyasema hayo wakati akikabidhi ripoti ya kamati yake kwa Rais John Magufuli leo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa gharama za shughuli za utafutaji na upembuzi madini nchini zimejumuishwa katika mauzo yake kwa kupunguza faida hivyo hawatozwi kodi. "Faida yote iliyopatikana katika uuzwaji wa dhahabu nje haikujumuishwa katika mahesabu ili kukwepa malipo ya mrabaha" alisema Prof. Osoro Ameongeza kuwa uchunguzi wa kamati yake umebaini kuwepo kwa utakatishwaji haramu wa fedha na faida kurudishwa kama mkopo kwa makampuni ya madini kitu ambacho ni kinyume cha taratibu.

KAMPUNI YA KUCHIMBA MADINI ACACIA ILIINGIA KINYEMELA NA HAINA KIBALI CHOCHOTE

Image
Taarifa ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi wa madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga wa madini iliyoundwa na Rais Joseph Magufuli, imebaini kuwa kampuni ya ACACIA Mining Plc haina kibali na inafanya kazi kinyume cha sheria.Prof. Osoro amesema kwamba Kamati yake imebaini kuwa Acacia haina uhalali wa kufanya shughuli zake hapa nchini na imetenda makosa yakiwemo kujipatia mali kwa udanganyifu, uhujumu uchumi, jinai na kuitia hasara taifa.Aidha Kamati ya Prof. Osoro imebaini kwamba Makinikia yaliyouzwa nje ya nchi hayakuwa makinikia hasa, bali yalikuwa ni madini mbalimbali huku ikiongeza kwamba katika mikataba ya uuzwaji wa makinikia hayo, serikali haikuwa sehemu ya mikataba hiyo.Prof. Osoro ameongeza kwamba jumla ya mapato yote ambayo serikali imepoteza ni Tsh. trilion 68.6 sawa na bajeti ya miaka miwili ya nchi kodi ya mapato ambayo taifa imepoteza ni Tsh. tril 55.07, mrahaba tril 11, bandari tril 1.6. na kwamba jumla ya thamani ya madini ...

MTOTO WA MIAKA 12, MOHAMED ABDULLAH AIBUKA MSHINDI MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAN BARANI AFRIKA

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi , Mohammed Abdullah Aden (12) wa Somalia hundi ya shilingi milioni 15, 750,000/= mshindi wa kwaza wa mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) MTOTO wa miaka 12 kutoka Somalia, Mohammed Abdullahi Aden ameibuka kidedea na kitita cha dola za Marekani 7,000 (sawa na sh. milioni 15.75) katika mashindano ya 18 ya Afrika ya kuhifadhi Quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30.  Mohammed ambaye ni miongoni mwa washiriki wadogo zaidi wawili kuliko wote (mwenzake anatoka Burundi), amejishindia pia IPAD, cheti, kompyuta iliyotolewa na Balozi wa Kuwait, ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na ahadi ya kwenda nchi yoyote aitakayo kutoka kwa kampuni ya Sky Bus Travel Agency ya jijini Dar es Salaam.  Akizungumza na maelfu ya waumini na Watanzania waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa j...

Fundi Seremala Mbaroni kwa kuwabaka binti zake

Image
FUNDI Seremala, Japhet Lendiman (38) mkazi wa Daraja Mbili, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, baada ya kubaka watoto wake wa kike wa darasa la sita na kidato cha kwanza. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kiini cha tatizo hilo ni nini na kufuatiwa na hatua ya kufikishwa mahakamani. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la polisi tangu Juni 6, mwaka huu na upelelezi unaendelea kubaini undani wa tukio hilo. Akimzungumzia mtuhumiwa huyo, mmoja wa majirani wa eneo hilo la Daraja Mbili (jina limehifadhiwa) alidai kuwa mzazi huyo amezoeleka kwa tabia hiyo mbaya mtaani kwao. Alidai kuwa mtuhumiwa huyo amezoea kubaka watoto wake mara kwa mara wakati mama yao akiwa kazini na kwamba Mei 28 majira ya saa 9:00 alasiri alimbaka tena mtoto wake (Jina tumelihifadhi) wa darasa la sita shule ya Msingi Daraja Mbili ndipo taarifa zilipoanza kuzagaa mtaani. “Siku hiyo ya tukio lililo...