Posts

Showing posts from February 12, 2018

Simba Hawaukosi Ubingwa

Image
KWA staili hii Simba inakosaje ubingwa wa Ligi Kuu Bara? Vigogo wa Simba wameibuka na kutangaza ofa mpya kwa wachezaji wa timu hiyo kwamba kila mechi watakayoshinda kila mchezaji atapata fedha ya maana. Simba hadi hivi sasa tayari imefanikiwa kushinda michezo 12 ya ligi kuu kati 17, ikitoka sare michezo mitano huku ikiwa haijapoteza mchezo wowote. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, wachezaji hao wameongezewa morali ya kupata ushindi na kuwawekea motisha ya fedha kwa kila mechi watakayoshinda ya ligi kuu na michuano ya kimataifa Afrika. Simba hivi sasa inawategemea zaidi Emmanuel Okwi na John Bocco katika kupata ushindi. Mtoa taarifa huyo alisema, motisha hiyo ya fedha imegawanywa kwa mafungu, ipo inayowahusisha wachezaji wa kikosi cha kwanza, akiba na wanaokaa ambao wao wanapata sawa. “Kiukweli hivi sasa mabosi na viongozi wa Simba, wamedhamiria kuuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu, kwani wameandaa motisha kwa wachezaji kwa kila me

KISA MNYETI, HECHE ASUBURI KAULI YA JPM

Image
MBUNGE wa Tarime Vijijini, John Heche amedai litakuwa jambo la ajabu kwa Watanzania kunyamazia ubaguzi unaofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ikiwa walikuwa mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi. Heche ametoa kauli hiyo mchana wa leo ikiwa ni muda mfupi baada ya taarifa za Mkuu huyo wa Mkoa kusambaa akiweka wazi wilayani Mbulu  kwamba hayuko tayari kutoa msaada kwa diwani wa chama cha upinzani kwa kuwa yeye anatekeleza ilani ya chama kilichopo madarakani. “ Kama Watanzania walikua mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi itakua jambo la ajabu kunyamazia ubaguzi na chuki ya Mnyeti dhidi ya Watanzania wengine, nasubiri kusikia kauli ya Chama chake na rais aliemteua Mnyeti.” alisema Heche.

Haya ndio mambo matatu waliozungumza Zitto Kabwe na Mh.Lissu Ubelgiji

Image
Jana Jumapili Februari 11, 2018 Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe alimtembelea Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Mhe Tundu Lissu ambaye yupo kwenye matibabu nchini Ubelgiji. Zitto Kabwe amesema kuwa walipokutana waligusia mambo makubwa matatu ambayo ni juu ya Gharama za matibabu yake, Suala la uchunguzi wa shambulio lake na maendeleo ya afya yake na mbinu za kuleta mabadiliko nchini. Kuhusu suala la matibabu Mhe. Zitto Kabwe amesema Lissu anasikitika kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka leo sio tu halimhudumii Lakini pia hata stahili zake za msingi kama Mbunge hapewi. Licha ya kutibiwa kwa misaada ya wasamaria wema, lakini ana mahitaji mengine kama mwanadam na wajibu kama mzazi. Sheria ya Bunge imeweka wazi kuwa Mbunge anapokuwa ametibiwa nje ya nchi Bunge humgharamia maisha yake. “Suala la Gharama za matibabu yake.,Lissu anasikitika kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka leo sio tu halimhudumii Lakini pia

Ajali Mbaya Yaua Sita Papo Hapo- Tanga

Image
WATU watano wamefariki dunia papo hapo na wengine sita kujeruhiwa vibaya, baada ya basi kubwa kugongana na Hiace katika eneo la Kabuku wilayani Handeni. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Leonce Rwegasira alisema ajali hiyo ilitoke saa 5:30 asubuhi katika eneo hilo la Kabuku. Alitaja magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni basi la Kampuni ya AJ Safari lililokuwa likitoka Lushoto kwenda Dar es Salaam likiendeshwa na Khalifa Mussa Omary mkazi wa Chamanzi Dar es Salaam lenye namba za usajili T 497 BJB mbalo limegongana na Hiace iliyokuwa ikitoka Mkata kwenda Segera yenye namba T591 AKE. Aliwataja waliokufa kuwa ni pamoja na dereva wa Hiace aliyefahamika kwa jina moja la Shabaan, wengine majina yao hayajatambulika na maiti zao zimehifadhiwa Kwenye Hospitali ya Magunga wilayani Korogwe. ACP Rwegasira alisema majeruhi ambao hawakuchukuliwa majina yao kutokana na uharaka wa kuwasaidia kuwafikisha katika Kituo cha Afya Kabuku kwa

'Maafisa Habari, TEHAMA ni Mawakala wa Mabadiliko’

Image
February 12, 2018 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara,Raphael Joseph Nyanda akifungua Semina kwa Maafisa hao wa Mkoa wa Mara na Arusha. Ndugu Wakili Mtebe, Meneja Mradi wa PS3, akiwakaribisha wageni wakati wa Ufunguzi. Mkuu wa Mawasiliano kutoka OR TAMISEMI, Bibi Rebecca Kwandu, akiteta jambo na Kaimu Katibu Tawala Mkoa muda mfupi kabla ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo. Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Raphael Joseph Nyanda, amewakumbusha Maafisa Habari na Maafisa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, maarifa na ubunifu, kwakuwa wao ni mawakala wa mabadiliko. Dkt. Peter Kilima, Mkurugenzi wa Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Wananchi kutoka PS3, akizungumza wakati wa Mafunzo hayo Akifungua kikao cha siku nne mkoani humo kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), Ndugu Nyanda amewatahadharish

Rais Magufuli afanya uteuzi huu

Image
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Omari Rashid Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) na Bw. Waziri Waziri Kindamba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo. Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa amesema kuwa Uteuzi wa Dkt. Omari Rashid Nundu na Bw. Waziri Waziri Kindamba umeanza tarehe 01 Februari, 2018. Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Omari Rashid Nundu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya iliyokuwa Kampuni ya Simu Tanzania (Tanzania Telecommunication Company Limited – TTCL) na Bw. Waziri Waziri Kindamba alikuwa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo. Pamoja na kufanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Mhe. Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwahamisha wafanyakazi wote na maafisa wa umma (Employees and Public Officers) wa iliyokuwa TTCL kwenda TTCL Corporation. Pia Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Ma